Milkah Wanjugu, J. N. Maitaria, Peter Kinyanjui Mwangi
{"title":"Matumizi ya Kinaya Kubainishia Maudhui katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Chozi la Heri na Tamthilia ya Kigogo","authors":"Milkah Wanjugu, J. N. Maitaria, Peter Kinyanjui Mwangi","doi":"10.37284/jammk.6.1.1303","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Mtunzi wa kazi ya kazi ya fasihi hususan riwaya na tamthilia, hutumia mbinu mahususi kuwasilishia matukio na mawazo yanavyoshuhudiwa katika jamii. Mbinu hizo huteuliwa na mtunzi kwa makusudi ili ujumbe unaokusudiwa kuwasilishwa na kueleweka kwa mwafaka na hadhira. Mbinu hizo ni zile zinazojibainisha katika kitengo cha tamathali za usemi. Katika utafiti huu, mbinu inayozingatiwa ni kinaya ambacho huwasilisha ujumbe kinyume na matarajio. Utafiti huu unatuonyesha matumizi ya kinaya katika riwaya ya Chozi la Heri (2017) ambayo imeandikwa na Matei na tamthilia ya Kigogo (2015) ambayo imeandikwa na Kea. Wanakejeli uhuru katika mataifa yaliyopata uhuru mwanzoni mwa miaka ya 1960 barani Afrika. Mataifa haya ni yale ambayo baada ya kupigania uhuru na kuunyakua kutoka kwa wakoloni, bado raia wanahisi kuwa wanaendelea kuwa katika hali ya kudhulumiwa na hali ya maisha kuwa magumu kutokana na uongozi usioafiki maono ya matarajio yao. Utafiti huu utabainisha jinsi watunzi wa riwaya na tamthilia teule yaani Assumpta Matei na Pauline Kea mtawalia walivyowasilisha kazi zao kwa kuzingatia mbinu ya kinaya katika kubainishia na kuukejeli uongozi katika bara la Afrika. Malengo ya utafiti huu yatakuwa, kufafanua matumizi ya kinaya katika riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo, kujadili jinsi waandishi wa riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo wametumia kinaya katika kuendeleza maudhui na kueleza jinsi mbinu ya kinaya ilivyotumiwa katika usawiri wa wahusika viongozi katika riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo. Utafiti huu utaongozwa na nadharia ya uhakiki wa mtindo na uchanganuzi wa data utaongozwa na mihimili ya nadharia hii kisha matokeo yatawasilishwa kwa njia ya maelezo.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"75 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-07-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1303","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Mtunzi wa kazi ya kazi ya fasihi hususan riwaya na tamthilia, hutumia mbinu mahususi kuwasilishia matukio na mawazo yanavyoshuhudiwa katika jamii. Mbinu hizo huteuliwa na mtunzi kwa makusudi ili ujumbe unaokusudiwa kuwasilishwa na kueleweka kwa mwafaka na hadhira. Mbinu hizo ni zile zinazojibainisha katika kitengo cha tamathali za usemi. Katika utafiti huu, mbinu inayozingatiwa ni kinaya ambacho huwasilisha ujumbe kinyume na matarajio. Utafiti huu unatuonyesha matumizi ya kinaya katika riwaya ya Chozi la Heri (2017) ambayo imeandikwa na Matei na tamthilia ya Kigogo (2015) ambayo imeandikwa na Kea. Wanakejeli uhuru katika mataifa yaliyopata uhuru mwanzoni mwa miaka ya 1960 barani Afrika. Mataifa haya ni yale ambayo baada ya kupigania uhuru na kuunyakua kutoka kwa wakoloni, bado raia wanahisi kuwa wanaendelea kuwa katika hali ya kudhulumiwa na hali ya maisha kuwa magumu kutokana na uongozi usioafiki maono ya matarajio yao. Utafiti huu utabainisha jinsi watunzi wa riwaya na tamthilia teule yaani Assumpta Matei na Pauline Kea mtawalia walivyowasilisha kazi zao kwa kuzingatia mbinu ya kinaya katika kubainishia na kuukejeli uongozi katika bara la Afrika. Malengo ya utafiti huu yatakuwa, kufafanua matumizi ya kinaya katika riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo, kujadili jinsi waandishi wa riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo wametumia kinaya katika kuendeleza maudhui na kueleza jinsi mbinu ya kinaya ilivyotumiwa katika usawiri wa wahusika viongozi katika riwaya ya Chozi la Heri na tamthilia ya Kigogo. Utafiti huu utaongozwa na nadharia ya uhakiki wa mtindo na uchanganuzi wa data utaongozwa na mihimili ya nadharia hii kisha matokeo yatawasilishwa kwa njia ya maelezo.