{"title":"Msatakabala na Changamoto za Kiswahili Nchini Uganda","authors":"F. Miima, Vincent Ferrel Kawoya","doi":"10.37284/jammk.3.1.367","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Kiswahili ni lugha ya kimataifa na ni mojawapo ya lugha rasmi za Muungano wa Nchi za Afrika. Vilevile, katika nchi za Afrika Mashariki, Kiswahili kina hadhi ya aina ya kipekee kikilinganishwa na lugha zingine zenye asili ya Kiafrika. Nchini Kenya na Tanzania ni lugha ya taifa na rasmi. Kwa upande mwingine, nchini Uganda, Kiswahili kinatambulika kikatiba kama lugha ya pili rasmi. Hali kadhalika katika kanda ya maziwa makuu kinategemewa sana kama chombo muhimu cha kufanikisha harakati za kibiashara. Kutokana na ukweli huu kuhusu hadhi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili, ingetarajiwa kuwa Kiswahili kingetumiwa kwa mawasiliano rasmi na katika ngazi mbalimbali za kimataifa. Hata hivyo, ni wazi kwamba kinakabiliwa na changamoto chungu nzima hasa zaidi nchini Uganda kiasi kwamba hatima yake haijulikani. Makala hii itaangazia hali ya lugha ya Kiswahili, changamoto zinazoikabili na hatima yake nchini Uganda. Itatoa mapendekezo kuhusu mikakati inayoweza kutumiwa ili kutamanisha wananchi wa Uganda kukienzi Kiswahili, kuinua hadhi yake na kukistawisha ipasavyo","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2021-07-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.3.1.367","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Kiswahili ni lugha ya kimataifa na ni mojawapo ya lugha rasmi za Muungano wa Nchi za Afrika. Vilevile, katika nchi za Afrika Mashariki, Kiswahili kina hadhi ya aina ya kipekee kikilinganishwa na lugha zingine zenye asili ya Kiafrika. Nchini Kenya na Tanzania ni lugha ya taifa na rasmi. Kwa upande mwingine, nchini Uganda, Kiswahili kinatambulika kikatiba kama lugha ya pili rasmi. Hali kadhalika katika kanda ya maziwa makuu kinategemewa sana kama chombo muhimu cha kufanikisha harakati za kibiashara. Kutokana na ukweli huu kuhusu hadhi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili, ingetarajiwa kuwa Kiswahili kingetumiwa kwa mawasiliano rasmi na katika ngazi mbalimbali za kimataifa. Hata hivyo, ni wazi kwamba kinakabiliwa na changamoto chungu nzima hasa zaidi nchini Uganda kiasi kwamba hatima yake haijulikani. Makala hii itaangazia hali ya lugha ya Kiswahili, changamoto zinazoikabili na hatima yake nchini Uganda. Itatoa mapendekezo kuhusu mikakati inayoweza kutumiwa ili kutamanisha wananchi wa Uganda kukienzi Kiswahili, kuinua hadhi yake na kukistawisha ipasavyo