{"title":"Tathmini ya Uamilifu wa Kiswahili Nchini Uganda: Mintarafu, Ueneaji wa Matumizi Yake Kwenye Asasi ya Uchapishaji","authors":"Abdu Salim Rais, Jacktone O. Onyango, I. Mbaabu","doi":"10.37284/jammk.5.1.641","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Kwa muda mrefu, Kiswahili kilifundishwa nchini Uganda kama taaluma ya Kigeni, licha ya kuwa lugha rasmi ya pili, baada ya Kiingereza (GoU, 1995). Hata hivyo, Kiswahili kina dhima kubwa katika asasi za muziki, ulinzi na elimu ambako Uamilifu wake unadhihirishwa na ueneaji wa matumizi yake (Mbaabu, 1991na Mlacha, 1995). Ingawa Kiswahili kilienea nchini Uganda, kabla ya kufikia mwishoni mwa wakati wa kukamilisha utafiti huu, viwango vya Uamilifu wake vilikuwa havijatathminiwa kitaaluma kupitia asasi ya uchapishaji. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa, kutathmini Uamilifu wa Kiswahili kutokana na ueneaji wa matumizi yake kupitia asasi ya Uchapishaji. Uamilifu wa Kiswahili ulichunguzwa kwa kutumia Nadharia ya Uamilifu iliyoasisiwa na Wanasosholojia Auguste Comte (1787-1857), Herbert Spencer (1830-1903), Vilfredo (1848-1917) na Emile Durkheim (1857-1917) na kuendelezwa na Mesthrie na wenzake (2004). Nadharia ya Uamilifu iliangazia jukumu lililotekelezwa na fani katika jamii mahsusi(Mesthrie et al., 2004).Kiini cha Uamilifu ni uwezekano wa kuweko kwa fani yenye vijisehemu mahsusi ambapo kila kijisehemu huchangia maendeleo kwa kutekeleza jukumu mahsusi katika fani hiyo (Mesthrie et al., 2004). Nadharia hiyo ilisaidia kutathmini dhima ya ueneaji wa matumizi ya Kiswahili kupitia Asasi ya Uchapishaji nchini Uganda. Istilahi Ueneaji hutokana na kitenzi enea chenye maana ya kuwa kila mahali. Kuenea katika muktadha huo, kulimaanisha kusambaa kwa matumizi ya Kiswahili nchini Uganda kwa kupitia asasi ya uchapishaji. Ueneaji ni hali ambapo fani fulani husambaa ijapokuwa muundo huweza kubadilika kulingana na mazingira. Wataalamu wa Ueneaji walishikilia kwamba, fani huweza kupenya kuta za kikabila na kuzagaa zaidi kutoka jamii zilizoendelea, kuelekea zisizoendelea (Buliba et al., 2014). Ithibati ni kwamba, fani za lugha za Watawala Wakoloni zinapatikana kwa wingi miongoni mwa Waafrika waliotawaliwa, na kinyume chake kikiwa sivyo (Buliba et al., 2014). Upeo wa utafiti huu ulikuwa Uchapishaji baina ya mwaka 2011 na 2018. Uchapishaji ni utoaji wa vitabu na kuvitawanya kwa kuviuzia watu (Bakita et al., 2012). Kihistoria, uchapishaji ulianzishwa nchini Uganda mnamo mwaka 1879 na Mmishonari Alexander Mackay wa ‘Church Missionary Society’ kwa madhumuni ya kufundisha Ukristo (Mbaabu, 1996). Kwa njia hiyo, uchapishaji wa kamusi na vitabu vya tafsiri za Biblia ulianzishwa kwa ajili ya kutaka kukidhi ufundishaji wake (Mbaabu, 2007). Ueneaji wa matumizi ya Kiswahili ulikadiriwa kutokana na ongezeko la Watumiaji wake nchini Uganda. Kwani ongezeko lilikomaa kiasi cha kuvuka mipaka ya awali (Myelimu, 2015). Taratibu za kithamano na kiwingi idadi zilitumika kwa kuzingatia mkabala wa pembe tatu kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data, iliyotokana na nyaraka za Wachapishaji pamoja na maoni ya Wahojiwa nyanjani. Data ilielezwa kwa kutumia asilimia za maratokezi za maoni ya Wahojiwa. Sampuli ya Wahojiwa wa hojaji ilitokana na Wadau wa Kiswahili wasiozidi 100 jijini Kampala. Sampuli hiyo ilibainishwa kupitia kwa kigezo cha Krejcie na Morgan, 1970, (Amin, 2005) kwa kutumia orodha ya Walimu kutokana na jukwaa la Chakitau. Sampuli ya wahojiwa wa ana kwa ana ambao ni Wataalamu na Wakuu wa mawanda iliteuliwa kimaksudi kupitia mbinu ya sampuli mkufu. Matokeo yataongeza maarifa mapya, kupanua upeo wa tafiti za baadaye, kuchangia swala la uteuzi lugha ya taifa na kupima dhima ya Kiswahili nchini Uganda.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"31 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-04-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.641","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Kwa muda mrefu, Kiswahili kilifundishwa nchini Uganda kama taaluma ya Kigeni, licha ya kuwa lugha rasmi ya pili, baada ya Kiingereza (GoU, 1995). Hata hivyo, Kiswahili kina dhima kubwa katika asasi za muziki, ulinzi na elimu ambako Uamilifu wake unadhihirishwa na ueneaji wa matumizi yake (Mbaabu, 1991na Mlacha, 1995). Ingawa Kiswahili kilienea nchini Uganda, kabla ya kufikia mwishoni mwa wakati wa kukamilisha utafiti huu, viwango vya Uamilifu wake vilikuwa havijatathminiwa kitaaluma kupitia asasi ya uchapishaji. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa, kutathmini Uamilifu wa Kiswahili kutokana na ueneaji wa matumizi yake kupitia asasi ya Uchapishaji. Uamilifu wa Kiswahili ulichunguzwa kwa kutumia Nadharia ya Uamilifu iliyoasisiwa na Wanasosholojia Auguste Comte (1787-1857), Herbert Spencer (1830-1903), Vilfredo (1848-1917) na Emile Durkheim (1857-1917) na kuendelezwa na Mesthrie na wenzake (2004). Nadharia ya Uamilifu iliangazia jukumu lililotekelezwa na fani katika jamii mahsusi(Mesthrie et al., 2004).Kiini cha Uamilifu ni uwezekano wa kuweko kwa fani yenye vijisehemu mahsusi ambapo kila kijisehemu huchangia maendeleo kwa kutekeleza jukumu mahsusi katika fani hiyo (Mesthrie et al., 2004). Nadharia hiyo ilisaidia kutathmini dhima ya ueneaji wa matumizi ya Kiswahili kupitia Asasi ya Uchapishaji nchini Uganda. Istilahi Ueneaji hutokana na kitenzi enea chenye maana ya kuwa kila mahali. Kuenea katika muktadha huo, kulimaanisha kusambaa kwa matumizi ya Kiswahili nchini Uganda kwa kupitia asasi ya uchapishaji. Ueneaji ni hali ambapo fani fulani husambaa ijapokuwa muundo huweza kubadilika kulingana na mazingira. Wataalamu wa Ueneaji walishikilia kwamba, fani huweza kupenya kuta za kikabila na kuzagaa zaidi kutoka jamii zilizoendelea, kuelekea zisizoendelea (Buliba et al., 2014). Ithibati ni kwamba, fani za lugha za Watawala Wakoloni zinapatikana kwa wingi miongoni mwa Waafrika waliotawaliwa, na kinyume chake kikiwa sivyo (Buliba et al., 2014). Upeo wa utafiti huu ulikuwa Uchapishaji baina ya mwaka 2011 na 2018. Uchapishaji ni utoaji wa vitabu na kuvitawanya kwa kuviuzia watu (Bakita et al., 2012). Kihistoria, uchapishaji ulianzishwa nchini Uganda mnamo mwaka 1879 na Mmishonari Alexander Mackay wa ‘Church Missionary Society’ kwa madhumuni ya kufundisha Ukristo (Mbaabu, 1996). Kwa njia hiyo, uchapishaji wa kamusi na vitabu vya tafsiri za Biblia ulianzishwa kwa ajili ya kutaka kukidhi ufundishaji wake (Mbaabu, 2007). Ueneaji wa matumizi ya Kiswahili ulikadiriwa kutokana na ongezeko la Watumiaji wake nchini Uganda. Kwani ongezeko lilikomaa kiasi cha kuvuka mipaka ya awali (Myelimu, 2015). Taratibu za kithamano na kiwingi idadi zilitumika kwa kuzingatia mkabala wa pembe tatu kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data, iliyotokana na nyaraka za Wachapishaji pamoja na maoni ya Wahojiwa nyanjani. Data ilielezwa kwa kutumia asilimia za maratokezi za maoni ya Wahojiwa. Sampuli ya Wahojiwa wa hojaji ilitokana na Wadau wa Kiswahili wasiozidi 100 jijini Kampala. Sampuli hiyo ilibainishwa kupitia kwa kigezo cha Krejcie na Morgan, 1970, (Amin, 2005) kwa kutumia orodha ya Walimu kutokana na jukwaa la Chakitau. Sampuli ya wahojiwa wa ana kwa ana ambao ni Wataalamu na Wakuu wa mawanda iliteuliwa kimaksudi kupitia mbinu ya sampuli mkufu. Matokeo yataongeza maarifa mapya, kupanua upeo wa tafiti za baadaye, kuchangia swala la uteuzi lugha ya taifa na kupima dhima ya Kiswahili nchini Uganda.