{"title":"Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi","authors":"Karuhanga Deusdedit, F. Indede","doi":"10.37284/jammk.6.1.1194","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi sana katika maisha ya mwanadamu kama vile kupoteza ujira, uharibikaji wa ndoa, maradhi ya zinaa, vifo, kukata tamaa na utengano miongoni mwa wanajamii. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: kubainisha usawiri wa ukahaba na wahusika makahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; kuchunguza sababu zinazowalazimu wahusika kufanya ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; na kudhihirisha athari za ukahaba kwa wahusika waliomo katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi. Mtafiti alitumia nadharia ya utekelezi ambayo ni miongoni mwa nadharia nyingi zenye mtazamo wa kisosholojia. Nadharia ya utekelezi imeendelezwa na wanasosholojia kama vile Talcort Parsons na Emile Durkheim kama wanavyonukuliwa na Worsely Introducing Sociology (1970), huku akisema kwamba ukahaba husababishwa na mambo mawili yaani haja ya kutekeleza mahitaji ya kiuchumi na kwa kukidhi matashi ya nafsi zao kiashki. Mtafiti pia alitumia nadharia ya umaksi iliyoanzishwa na Karl Marx (1818-1863) na Fredrich Engles(1820-1895). Nadharia hii hufaa utafiti huu kwa kudhihirisha wahusika wanaoshiriki katika vitendo vya ukahaba kwa ajili ya kupata fedha au zawadi. Mabepari au walionacho huwa na lengo la kuridhisha miili yao tu na wanyonge huwa na lengo la kupata pesa ili kutimiza mahitaji yao, pengine, mnyonge hutolea mwili wake kwa ajili ya kupewa kazi au kupandishwa cheo kazini au kama njia ya kuilinda kazi yake ili asipigwe kalamu. Utafiti huu ni wa maktabani kwa hivyo, maktaba yaliyotumika ni yale ya Chuo Kikuu cha uislamu kilichopo nchini Uganda, Chuo kikuu cha Bishop Stuart Mbarara, na maktabani ya shule ya upili Heritage. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uchunguzaji wa riwaya teule yaani: ile ya Nyota ya Rehema na ya Ndoto ya Almasi kwa kuzisoma na kuzichambua kwa kina na kuiwasilishwa data kwa mbinu ya kiuthamano. Utafiti huu umebainisha kuwa wahusika hufanya ukahaba ili kupata pesa au kuridhisha matashi ya nafsi zao kiashiki. Utafiti huu utakuwa wa muhimu sana kwa kufunza jamii kwamba kahaba si mwanamke peke yake kama inavyochukuliwa katika baadhi ya jamii bali kahaba ni mtu yeyote awe mwanamume au mwanamke anayeshiririki vitendo vya uzinzi.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"130 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-05-01","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1194","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi sana katika maisha ya mwanadamu kama vile kupoteza ujira, uharibikaji wa ndoa, maradhi ya zinaa, vifo, kukata tamaa na utengano miongoni mwa wanajamii. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni: kubainisha usawiri wa ukahaba na wahusika makahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; kuchunguza sababu zinazowalazimu wahusika kufanya ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi; na kudhihirisha athari za ukahaba kwa wahusika waliomo katika riwaya ya Nyota ya Rehema na Ndoto ya Almasi. Mtafiti alitumia nadharia ya utekelezi ambayo ni miongoni mwa nadharia nyingi zenye mtazamo wa kisosholojia. Nadharia ya utekelezi imeendelezwa na wanasosholojia kama vile Talcort Parsons na Emile Durkheim kama wanavyonukuliwa na Worsely Introducing Sociology (1970), huku akisema kwamba ukahaba husababishwa na mambo mawili yaani haja ya kutekeleza mahitaji ya kiuchumi na kwa kukidhi matashi ya nafsi zao kiashki. Mtafiti pia alitumia nadharia ya umaksi iliyoanzishwa na Karl Marx (1818-1863) na Fredrich Engles(1820-1895). Nadharia hii hufaa utafiti huu kwa kudhihirisha wahusika wanaoshiriki katika vitendo vya ukahaba kwa ajili ya kupata fedha au zawadi. Mabepari au walionacho huwa na lengo la kuridhisha miili yao tu na wanyonge huwa na lengo la kupata pesa ili kutimiza mahitaji yao, pengine, mnyonge hutolea mwili wake kwa ajili ya kupewa kazi au kupandishwa cheo kazini au kama njia ya kuilinda kazi yake ili asipigwe kalamu. Utafiti huu ni wa maktabani kwa hivyo, maktaba yaliyotumika ni yale ya Chuo Kikuu cha uislamu kilichopo nchini Uganda, Chuo kikuu cha Bishop Stuart Mbarara, na maktabani ya shule ya upili Heritage. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na uchunguzaji wa riwaya teule yaani: ile ya Nyota ya Rehema na ya Ndoto ya Almasi kwa kuzisoma na kuzichambua kwa kina na kuiwasilishwa data kwa mbinu ya kiuthamano. Utafiti huu umebainisha kuwa wahusika hufanya ukahaba ili kupata pesa au kuridhisha matashi ya nafsi zao kiashiki. Utafiti huu utakuwa wa muhimu sana kwa kufunza jamii kwamba kahaba si mwanamke peke yake kama inavyochukuliwa katika baadhi ya jamii bali kahaba ni mtu yeyote awe mwanamume au mwanamke anayeshiririki vitendo vya uzinzi.