Kimathi Mwembu, Allan Mugambi, Timothy Kinoti M’Ngaruthi
{"title":"Ubadili Maana katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Kifonolojia na Kimofolojia","authors":"Kimathi Mwembu, Allan Mugambi, Timothy Kinoti M’Ngaruthi","doi":"10.37284/jammk.5.1.860","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji, uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"16 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-09-26","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.860","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji, uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia.