{"title":"Dhima ya Matambiko katika Jamii ya Waturkana","authors":"Hosea Lorot Gogong","doi":"10.37284/jammk.5.2.992","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala hii inabainisha kuwa jamii ya Waturkana hutekeleza matambiko aina tofauti tofauti. Aidha, matambiko hayo huwa na dhima kubwa katika jamii hiyo. Stadi hii ilichochewa na haja ya kupigania nafasi stahili ya fasihi ya Mwafrika hususan nafasi ya matambiko katika tamaduni ya Waafrika. Makala hii itabaini na kuthibitisha kuwa, Matambiko yana nafasi muhimu sana katika fasihi ya jamii ya Waturkana. Pia, utafiti huu utathibitisha ufasihi wa matambiko. Nadharia za uhalisiajabu zilimwongoza mtafiti kuchunguza suala la matambiko katika jamii ya Waturkana. Pia, nadharia ya utendaji ilimsaidia mtafiti kuchunguza suala la utendaji wakati wa kutambika. Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Data kuhusu aina za matambiko na dhima yake ilikusanywa kutoka maktabani na nyanjani. Ili kuafikia lengo kuu, mbinu mbalimbali za ukusanyaji data zilitumika ambazo ni mahojiano, usikilizaji, utazamaji na unukuzi daftarini. Sampuli ziliteuliwa kimaksudi, mtafiti alitumia mtindo wa sampuli azimiwa katika kuwateua wazee ishirini na saba (27), wazee wa kiume kumi na nane (18) na wa kike tisa (9) kutoka katika vijiji tisa ambazo ni Kaenyumae, Moru-lingakirion, Nagetei, Loreng, Nareng-munyen, Nakimak, Edos, Kapoong, na Kadokochini. Wazee wa kiume wawili na wa kike mmoja waliteuliwa kutoka katika kila Kijiji. Vijiji hivi vinapatikana kwenye kata ndogo ya Locher-emoit iliyoko kwenye kata ya Lochwaa-Ngikamatak, eneo la Kaunti ndogo ya Turkana Kusini kwenye Kaunti ya Turkana. Idadi kubwa ya wakazi wa Kaunti ya Turkana ni Waturkana. Isitoshe, umri wa wazee walioteuliwa ulikuwa kuanzia miaka hamsini na tano kwenda mbele. Kigezo cha umri kilitumika kwa sababu inaaminika kuwa wazee wa umri huo ndio wana tajriba katika mchakato mzima wa utekelezaji wa matambiko. Kwa mujibu wa Ramsay (2005), data zilizokusanywa kutokana na mahojiano zilichanganuliwa kwa kuzingatia uchanganuzi wa kithamano. Aidha, data za utafiti huu ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa jamii ya Waturkana hutambika na huwa na matambiko ya aina tofauti tofauti. Isitoshe, utafiti huu umesaidia kukusanya data kuhusu matambiko na kuzihifadhi katika maandishi, kwani mambo mengi ya Fasihi Simulizi ya jamii ya Waturkana bado yamehifadhiwa vichwani mwa watu kama sehemu ya kutunzia kumbukumbu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"14 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-12-05","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.2.992","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala hii inabainisha kuwa jamii ya Waturkana hutekeleza matambiko aina tofauti tofauti. Aidha, matambiko hayo huwa na dhima kubwa katika jamii hiyo. Stadi hii ilichochewa na haja ya kupigania nafasi stahili ya fasihi ya Mwafrika hususan nafasi ya matambiko katika tamaduni ya Waafrika. Makala hii itabaini na kuthibitisha kuwa, Matambiko yana nafasi muhimu sana katika fasihi ya jamii ya Waturkana. Pia, utafiti huu utathibitisha ufasihi wa matambiko. Nadharia za uhalisiajabu zilimwongoza mtafiti kuchunguza suala la matambiko katika jamii ya Waturkana. Pia, nadharia ya utendaji ilimsaidia mtafiti kuchunguza suala la utendaji wakati wa kutambika. Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Data kuhusu aina za matambiko na dhima yake ilikusanywa kutoka maktabani na nyanjani. Ili kuafikia lengo kuu, mbinu mbalimbali za ukusanyaji data zilitumika ambazo ni mahojiano, usikilizaji, utazamaji na unukuzi daftarini. Sampuli ziliteuliwa kimaksudi, mtafiti alitumia mtindo wa sampuli azimiwa katika kuwateua wazee ishirini na saba (27), wazee wa kiume kumi na nane (18) na wa kike tisa (9) kutoka katika vijiji tisa ambazo ni Kaenyumae, Moru-lingakirion, Nagetei, Loreng, Nareng-munyen, Nakimak, Edos, Kapoong, na Kadokochini. Wazee wa kiume wawili na wa kike mmoja waliteuliwa kutoka katika kila Kijiji. Vijiji hivi vinapatikana kwenye kata ndogo ya Locher-emoit iliyoko kwenye kata ya Lochwaa-Ngikamatak, eneo la Kaunti ndogo ya Turkana Kusini kwenye Kaunti ya Turkana. Idadi kubwa ya wakazi wa Kaunti ya Turkana ni Waturkana. Isitoshe, umri wa wazee walioteuliwa ulikuwa kuanzia miaka hamsini na tano kwenda mbele. Kigezo cha umri kilitumika kwa sababu inaaminika kuwa wazee wa umri huo ndio wana tajriba katika mchakato mzima wa utekelezaji wa matambiko. Kwa mujibu wa Ramsay (2005), data zilizokusanywa kutokana na mahojiano zilichanganuliwa kwa kuzingatia uchanganuzi wa kithamano. Aidha, data za utafiti huu ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa jamii ya Waturkana hutambika na huwa na matambiko ya aina tofauti tofauti. Isitoshe, utafiti huu umesaidia kukusanya data kuhusu matambiko na kuzihifadhi katika maandishi, kwani mambo mengi ya Fasihi Simulizi ya jamii ya Waturkana bado yamehifadhiwa vichwani mwa watu kama sehemu ya kutunzia kumbukumbu.