{"title":"Motifu ya Ukame katika Tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015)","authors":"Mary K. Njeru, John M. Kobia, Dorcas M. Musyimi","doi":"10.37284/jammk.5.1.733","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Suala la ukame limeanza kupata umakini mwingi kwa sababu ya kuongezeka kwa hivi karibuni kwa marudio na makali yake. Mathalani, ni mwanzo wa maafa yanayoaminika kuwa chanzo cha kimsingi cha baa la njaa kwa ajili ya uharibifu wa mazao. Kadhalika, ni kutokana na makali ya ukame katika mataifa mbalimbali Barani Afrika na ulimwenguni kwa jumla, ambapo kumeibuka mijadala mizito miongoni mwa washikadau mbalimbali wa masuala ya kimazingira kote ulimwenguni. Tangu kuvumbuliwa kwa uwanja wa fasihi mazingira miaka ya tisini, waandishi wa kifasihi wamejihusisha katika masuala ya kimazingira ili kuchangia katika utatuzi wa matatizo yanayotokana na uharibifu wa mazingira. Kwa msingi huu, makala hii inajadili namna watunzi wa tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015) wamesawiri motifu ya ukame kama suala mojawapo la kimazingira kwa lengo la kuweka wazi chanzo na athari zake katika jamii. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Nadharia hii hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Utafiti ulifanyiwa maktabani ambapo uteuzi wa sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua matini teule. Data ya utafiti ilikusanywa kupitia usomaji wa kina wa matini teule. Kutokana na matokeo ya makala hii, ilibainika kwamba, waandishi wa tamthilia teule wamesawiri suala la ukame kwa namna mbalimbali kwa kuangazia chanzo na athari zake. Hivyo, makala hii imethibitisha kwamba, fasihi ya Kiswahili ni nyenzo muhimu ambayo inaweza kutumika katika kuangazia masuala yanayoathiri jamii. Vilevile, utafiti huu ni muhimu kwa washikadau wote wa masuala ya kimazingira Barani Afrika na ulimwengu kwa jumla.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"139 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-07-04","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.733","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Suala la ukame limeanza kupata umakini mwingi kwa sababu ya kuongezeka kwa hivi karibuni kwa marudio na makali yake. Mathalani, ni mwanzo wa maafa yanayoaminika kuwa chanzo cha kimsingi cha baa la njaa kwa ajili ya uharibifu wa mazao. Kadhalika, ni kutokana na makali ya ukame katika mataifa mbalimbali Barani Afrika na ulimwenguni kwa jumla, ambapo kumeibuka mijadala mizito miongoni mwa washikadau mbalimbali wa masuala ya kimazingira kote ulimwenguni. Tangu kuvumbuliwa kwa uwanja wa fasihi mazingira miaka ya tisini, waandishi wa kifasihi wamejihusisha katika masuala ya kimazingira ili kuchangia katika utatuzi wa matatizo yanayotokana na uharibifu wa mazingira. Kwa msingi huu, makala hii inajadili namna watunzi wa tamthilia za Janga la Werevu (Mohamed, 2011) na Majira ya Utasa (Arege, 2015) wamesawiri motifu ya ukame kama suala mojawapo la kimazingira kwa lengo la kuweka wazi chanzo na athari zake katika jamii. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Nadharia hii hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Utafiti ulifanyiwa maktabani ambapo uteuzi wa sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua matini teule. Data ya utafiti ilikusanywa kupitia usomaji wa kina wa matini teule. Kutokana na matokeo ya makala hii, ilibainika kwamba, waandishi wa tamthilia teule wamesawiri suala la ukame kwa namna mbalimbali kwa kuangazia chanzo na athari zake. Hivyo, makala hii imethibitisha kwamba, fasihi ya Kiswahili ni nyenzo muhimu ambayo inaweza kutumika katika kuangazia masuala yanayoathiri jamii. Vilevile, utafiti huu ni muhimu kwa washikadau wote wa masuala ya kimazingira Barani Afrika na ulimwengu kwa jumla.