{"title":"Changamoto Zinazowakabili Wanafunzi Wakimbizi wa Sudan Kusini katika Ushairi wa Kiswahili","authors":"E. E. Lokidor","doi":"10.37284/jammk.6.1.1106","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Utafiti huu unaeleza changamoto zinazowakumba wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini katika ushairi wa Kiswahili. Utafiti huu ulilenga kuchunguza changamoto zinazokumba wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini katika ushairi wa Kiswahili katika shule ya upili. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa ilielekeza utafiti huu. Utafiti huu ulifanywa katika shule ya upili ya Fanaka (jina la msimbo) katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Data ilikusanywa kupitia mahojiano, uchunzaji na uchanganuzi wa matini. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanakabiliwa na changamoto ya ugumu wa kujibu maswali ya ushairi. Changamoto ya ugumu wa ushairi kwa wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini imetokana na mtazamo hasi kuwa ushairi ni mgumu, ukosefu wa miongozo ya ushairi, ukosefu wa vitabu teule vya ushairi, na walimu kutotumia mbinu na nyenzo mwafaka za kufundisha ushairi. Utafiti umetoa mapendekezo ya jinsi ya kuboresha ufundishaji wa ushairi katika shule za upili nchini Kenya. Aidha, utafiti huu unatoa mchango kwa ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili kwa wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"27 1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-02-23","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1106","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Utafiti huu unaeleza changamoto zinazowakumba wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini katika ushairi wa Kiswahili. Utafiti huu ulilenga kuchunguza changamoto zinazokumba wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini katika ushairi wa Kiswahili katika shule ya upili. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa ilielekeza utafiti huu. Utafiti huu ulifanywa katika shule ya upili ya Fanaka (jina la msimbo) katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Data ilikusanywa kupitia mahojiano, uchunzaji na uchanganuzi wa matini. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanakabiliwa na changamoto ya ugumu wa kujibu maswali ya ushairi. Changamoto ya ugumu wa ushairi kwa wanafunzi wakimbizi kutoka Sudan Kusini imetokana na mtazamo hasi kuwa ushairi ni mgumu, ukosefu wa miongozo ya ushairi, ukosefu wa vitabu teule vya ushairi, na walimu kutotumia mbinu na nyenzo mwafaka za kufundisha ushairi. Utafiti umetoa mapendekezo ya jinsi ya kuboresha ufundishaji wa ushairi katika shule za upili nchini Kenya. Aidha, utafiti huu unatoa mchango kwa ufundishaji na ujifunzaji wa ushairi wa Kiswahili kwa wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili