{"title":"Dhima ya Usimulizi Katika Uwasilishaji wa Nyimbo za Taarab: Uchunguzi wa Kipengele cha Wakati","authors":"Dorcas Misoi, R. M. Wafula","doi":"10.37284/jammk.5.1.702","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Taarab ni aina ya nyimbo yenye asili katika Pwani ya Afrika Mashariki. Nyimbo hizi kama zilivyo nyimbo zingine, ni zao la shughuli na hisia za binadamu. Hivyo, ujumbe katika nyimbo hizo hujikita katika miktadha mbalimbali ya jamii. Ntarangwi (2001) anasema, mbali na kuwa nyimbo za taarab huimbwa sana katika harusi za Waswahili, nyingi ya nyimbo hizo hugusia masuala mengine ya maisha kama vile uongozi, dini, urembo wa wanawake, mabadiliko ya kisiasa au hata kuhusu uchungu wa kumpoteza mpenzi. Masuala haya huwasilishwa na watribu kwa kutumia mbinu za lugha kwa ubunifu wa kiwango cha juu. Makala haya yamechunguza dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa nyimbo za taarab kwa kuzingatia kipengele mahsusi cha wakati. Kazi hii imeongozwa na nadharia ya naratolojia inayohusishwa na mwanafalsafa wa Kiyunani aitwaye Plato na kuendelezwa na wataalamu kama vile Genette, Stanzel, Manfred Jan na Mieke Bal. Nadharia hii inahusu usimuliaji wa hadithi. Misingi yake ni kuwa usimulizi lazima uwe na msimulizi, kitendo kinachosimuliwa, usemi kuhusu kinachofanyika, wahusika na dhamira ya usimulizi wowote hubainika kupitia kwa mtazamo wa msimulizi. Kipengele cha usimulizi cha wakati kimetumiwa kuonyesha dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa maudhui na mtindo wa uwasilishi katika nyimbo za taarab. Katika kufanya hivyo, makala haya yamebainisha kuwa kipengele cha usimulizi cha wakati kimedhihirika katika nyimbo teule za taarab na kimechangia kukuza maudhui na mtindo wa uwasilishi kwa kuonyesha kuwa wimbo wa taarab ni utanzu telezi unaosheheni usimulizi","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"22 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-06-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.702","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Taarab ni aina ya nyimbo yenye asili katika Pwani ya Afrika Mashariki. Nyimbo hizi kama zilivyo nyimbo zingine, ni zao la shughuli na hisia za binadamu. Hivyo, ujumbe katika nyimbo hizo hujikita katika miktadha mbalimbali ya jamii. Ntarangwi (2001) anasema, mbali na kuwa nyimbo za taarab huimbwa sana katika harusi za Waswahili, nyingi ya nyimbo hizo hugusia masuala mengine ya maisha kama vile uongozi, dini, urembo wa wanawake, mabadiliko ya kisiasa au hata kuhusu uchungu wa kumpoteza mpenzi. Masuala haya huwasilishwa na watribu kwa kutumia mbinu za lugha kwa ubunifu wa kiwango cha juu. Makala haya yamechunguza dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa nyimbo za taarab kwa kuzingatia kipengele mahsusi cha wakati. Kazi hii imeongozwa na nadharia ya naratolojia inayohusishwa na mwanafalsafa wa Kiyunani aitwaye Plato na kuendelezwa na wataalamu kama vile Genette, Stanzel, Manfred Jan na Mieke Bal. Nadharia hii inahusu usimuliaji wa hadithi. Misingi yake ni kuwa usimulizi lazima uwe na msimulizi, kitendo kinachosimuliwa, usemi kuhusu kinachofanyika, wahusika na dhamira ya usimulizi wowote hubainika kupitia kwa mtazamo wa msimulizi. Kipengele cha usimulizi cha wakati kimetumiwa kuonyesha dhima ya usimulizi katika uwasilishaji wa maudhui na mtindo wa uwasilishi katika nyimbo za taarab. Katika kufanya hivyo, makala haya yamebainisha kuwa kipengele cha usimulizi cha wakati kimedhihirika katika nyimbo teule za taarab na kimechangia kukuza maudhui na mtindo wa uwasilishi kwa kuonyesha kuwa wimbo wa taarab ni utanzu telezi unaosheheni usimulizi