{"title":"Maumbo na Maana za Majina ya Asili ya Watu Katika Jamii-lugha ya Wagogo","authors":"Jemima Lenjima, Julius Edmund Frank","doi":"10.37284/jammk.6.1.1271","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala haya yamechunguza maumbo na maana za majina ya asili ya watu katika jamii-lugha ya Wagogo kwa kuchanganua vijenzi mbalimbali vinavyojenga majina hayo. Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa kutoka katika wilaya ya Mpwapwa na Chamwino, mkoani Dodoma kwa ajili ya tasnifu ya Uzamivu. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika kwa mujibu wa Kiparsky (1982) inayosisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno vimepangwa kidarajia kimsonge ambapo vipashio vidogo huungana ili kuunda vipashio vikubwa. Data za makala haya zimewasilishwa kwa majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwa kwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika na kuonesha jinsi vipashio hivyo vilivyopangwa kidarajia kimsonge. Matokeo ya uchanganuzi huo yamedhihirisha kuwa majina ya asili ya watu yaliyochunguzwa yameundwa kwa vijenzi mbalimbali ambavyo vimechanganuliwa kimofolojia na kuleta maana. Tofauti na baadhi ya wanaisimu wanaodai kuwa majina ya watu yameundwa na mzizi au mashina tu, makala haya yamedhihirisha kuwa vipo vipashio maalumu vinayounda majina ya asili ya watu na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"13 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-06-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1271","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala haya yamechunguza maumbo na maana za majina ya asili ya watu katika jamii-lugha ya Wagogo kwa kuchanganua vijenzi mbalimbali vinavyojenga majina hayo. Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa kutoka katika wilaya ya Mpwapwa na Chamwino, mkoani Dodoma kwa ajili ya tasnifu ya Uzamivu. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika kwa mujibu wa Kiparsky (1982) inayosisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno vimepangwa kidarajia kimsonge ambapo vipashio vidogo huungana ili kuunda vipashio vikubwa. Data za makala haya zimewasilishwa kwa majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwa kwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika na kuonesha jinsi vipashio hivyo vilivyopangwa kidarajia kimsonge. Matokeo ya uchanganuzi huo yamedhihirisha kuwa majina ya asili ya watu yaliyochunguzwa yameundwa kwa vijenzi mbalimbali ambavyo vimechanganuliwa kimofolojia na kuleta maana. Tofauti na baadhi ya wanaisimu wanaodai kuwa majina ya watu yameundwa na mzizi au mashina tu, makala haya yamedhihirisha kuwa vipo vipashio maalumu vinayounda majina ya asili ya watu na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia