{"title":"Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi","authors":"Harrison Onyango Ogutu","doi":"10.37284/jammk.5.1.686","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala hii imechunguza suala la propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika riwaya teule za Kiswahili. Mtafiti amejadili namna propaganda inatumiwa kudumisha na kuimarisha utawala wa viongozi mintarafu ya riwaya teule. Ili kutimiza lengo lake, mtafiti amehakiki riwaya nne: Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi. Nadharia ya hejemonia inayoweka wazi suala la utawala wa mabwanyenye juu ya raia na kueleza udumishaji wa uwezo na mamlaka juu ya watawaliwa ni mwafaka katika utafiti huu. Mintarafu ya nadharia hii, hejemonia huendelezwa na kudumishwa sio tu kwa ushurutishaji bali pia kupitia maafikiano, lugha, wataalamu, siasa, maagizo, burudani, ujumbe na nyenzo nyingine za kielimu. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudi kwa kudhamiria kuwa zimesheheni masuala ya uhimili wa hejemonia. Kutokana na riwaya hizo, mtafiti alipata mitazamo mipana na tofauti ya propaganda kwa mujibu wa nguzo za nadharia na madhumuni ya utafiti. Utafiti huu ni wa maktabani ambako usomi mpana na wa kina wa riwaya teule, vitabu vya ziada, majarida na tasnifu mbalimbali ulitekelezwa. Utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kiuthamano ikitumika kuchanganua data hiyo. Muundo wa kimaelezi ulitumika kuchanganua data na kueleza matukio kwa uyakinifu. Utafiti umeonesha kuwa propaganda ni mkakati muhimu unaotumiwa na watu wenye uwezo na mamlaka kudumisha na kuhimili hejemonia katika jamii. Matokeo ya utafiti yanatoa maarifa zaidi kuhusu matumizi ya propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika fasihi. Aidha, matokeo haya ni marejeleo muhimu kwa wahakiki na watafiti hususan wale wanaotafitia masuala ya hejemonia katika fasihi","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"31 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-05-30","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.686","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala hii imechunguza suala la propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika riwaya teule za Kiswahili. Mtafiti amejadili namna propaganda inatumiwa kudumisha na kuimarisha utawala wa viongozi mintarafu ya riwaya teule. Ili kutimiza lengo lake, mtafiti amehakiki riwaya nne: Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi. Nadharia ya hejemonia inayoweka wazi suala la utawala wa mabwanyenye juu ya raia na kueleza udumishaji wa uwezo na mamlaka juu ya watawaliwa ni mwafaka katika utafiti huu. Mintarafu ya nadharia hii, hejemonia huendelezwa na kudumishwa sio tu kwa ushurutishaji bali pia kupitia maafikiano, lugha, wataalamu, siasa, maagizo, burudani, ujumbe na nyenzo nyingine za kielimu. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudi kwa kudhamiria kuwa zimesheheni masuala ya uhimili wa hejemonia. Kutokana na riwaya hizo, mtafiti alipata mitazamo mipana na tofauti ya propaganda kwa mujibu wa nguzo za nadharia na madhumuni ya utafiti. Utafiti huu ni wa maktabani ambako usomi mpana na wa kina wa riwaya teule, vitabu vya ziada, majarida na tasnifu mbalimbali ulitekelezwa. Utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kiuthamano ikitumika kuchanganua data hiyo. Muundo wa kimaelezi ulitumika kuchanganua data na kueleza matukio kwa uyakinifu. Utafiti umeonesha kuwa propaganda ni mkakati muhimu unaotumiwa na watu wenye uwezo na mamlaka kudumisha na kuhimili hejemonia katika jamii. Matokeo ya utafiti yanatoa maarifa zaidi kuhusu matumizi ya propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika fasihi. Aidha, matokeo haya ni marejeleo muhimu kwa wahakiki na watafiti hususan wale wanaotafitia masuala ya hejemonia katika fasihi