{"title":"Utaratibu wa Vipengele vya Kirai Nomino katika Kiswahili","authors":"Chege Joel Ngari, Leonard Chacha Mwita","doi":"10.37284/jammk.5.1.826","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Lugha zote ulimwenguni huwa na sheria zake zinazohusu mfuatano wa maneno katika sentensi. Hivyo basi, kama zilivyo lugha zingine, lugha ya Kiswahili vilevile ina utaratibu mwafaka ambao vivumishi katika kirai nomino (KN) hufuata ili kuibua sentensi kubalifu sio kimantiki tu, bali pia kisarufi, jambo ambalo huathiri maana ya KN husika. Makala haya yameweka bayana utaratibu wa vipengele vya kirai nomino katika Kiswahili. Nadharia ya Eksibaa iliyoasisiwa na Noam Chomsky ilitumika. Nadharia ya Eksibaa ni nadharia ya muundo virai inayoonyesha kategoria za sintaksia zinazofungamanishwa na nomino. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni hojaji na mahojiano. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu husika zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikifidia mapungufu ya nyingine. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio. Utafiti huu ulishirikisha watafitiwa 120 ili kuafiki lengo husika. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makundi matatu ya utaratibu wa vipengele vya kirai nomino ambayo ni: kirai nomino cha kiwakilishi na vivumishi, kirai nomino chenye nomino vivumishi na kishazi tegemezi na mwisho ni kirai nomino cha nomino, kitenzi jina na kivumishi. Matokeo ya utafiti huu yatapanua uelewa wa kirai nomino kwa mitazamo tofauti na hivyo kuongeza maarifa kuhusiana na dhana husika. Vilevile, mapendekezo ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa wanafunzi, waandishi wa vitabu, Wizara ya Elimu, serikali, wapangaji mitaala, watafiti wa baadaye na walimu chipukizi kupanua ufahamu na uelewa wa tawi la isimu ambalo ni pragmatiki.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"18 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-09-05","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.826","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Lugha zote ulimwenguni huwa na sheria zake zinazohusu mfuatano wa maneno katika sentensi. Hivyo basi, kama zilivyo lugha zingine, lugha ya Kiswahili vilevile ina utaratibu mwafaka ambao vivumishi katika kirai nomino (KN) hufuata ili kuibua sentensi kubalifu sio kimantiki tu, bali pia kisarufi, jambo ambalo huathiri maana ya KN husika. Makala haya yameweka bayana utaratibu wa vipengele vya kirai nomino katika Kiswahili. Nadharia ya Eksibaa iliyoasisiwa na Noam Chomsky ilitumika. Nadharia ya Eksibaa ni nadharia ya muundo virai inayoonyesha kategoria za sintaksia zinazofungamanishwa na nomino. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni hojaji na mahojiano. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu husika zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikifidia mapungufu ya nyingine. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio. Utafiti huu ulishirikisha watafitiwa 120 ili kuafiki lengo husika. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makundi matatu ya utaratibu wa vipengele vya kirai nomino ambayo ni: kirai nomino cha kiwakilishi na vivumishi, kirai nomino chenye nomino vivumishi na kishazi tegemezi na mwisho ni kirai nomino cha nomino, kitenzi jina na kivumishi. Matokeo ya utafiti huu yatapanua uelewa wa kirai nomino kwa mitazamo tofauti na hivyo kuongeza maarifa kuhusiana na dhana husika. Vilevile, mapendekezo ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa wanafunzi, waandishi wa vitabu, Wizara ya Elimu, serikali, wapangaji mitaala, watafiti wa baadaye na walimu chipukizi kupanua ufahamu na uelewa wa tawi la isimu ambalo ni pragmatiki.