{"title":"Usawiri wa Motifu za Kimazingira Katika Tamthilia ya Kiswahili: Tathmini ya Majira ya Utasa (Arege, 2015)","authors":"Mary K. Njeru, John M. Kobia, Dorcas M. Musyimi","doi":"10.37284/jammk.5.1.699","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Suala la kuongezeka kwa viwango vya halijoto na mabadiliko ya tabianchi limeibua mijadala ya kitaifa na kimataifa. Kwa msingi huu, kazi mbalimbali za kifasihi zimebuniwa kwa kuangazia uharibifu wa mazingira asilia na athari zake na mwito wa kuhifadhi mazingira. Makala hii ilikusudia kuchunguza jinsi motifu za kimazingira zilivyosawiriwa katika tamthilia ya Majira ya Utasa (Arege, 2015). Msisitizo ulikuwa kuangazia jinsi mwandishi wa tamthilia teule amesawiri motifu za kimazingira ili kuonyesha uharibifu wa mazingira pamoja na matatizo yanayotokana na uharibifu huo. Hii ni kwa sababu fasihi huwasilisha hali, maingiliano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira. Kwa hivyo, ni mojawapo ya nyenzo inayoweza kuchangia katika kuangazia matatizo yanayokumba jamii yoyote iwayo. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Kimsingi, nadharia ya uhakiki wa kiekolojia hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Tamthilia iliyohakikiwa iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake makuu yanahusiana moja kwa moja na mada ya makala hii. Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia usomaji wa kina wa tamthilia teule. Matokeo ya makala hii yalithibitisha kuwa mwandishi wa tamthilia ya Majira ya Utasa amesawiri motifu za kimazingira kwa namna mbalimbali kwa kuonyesha njia za uharibifu wa mazingira na athari zake. Hivyo, kushadidia kuwa fasihi inaakisi kikamilifu matatizo yanayoibuka katika jamii ilimoibuka. Kwa hivyo, ni chombo madhubuti kinachoweza kutumiwa kutatua matatizo hayo.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"164 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-06-10","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.699","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Suala la kuongezeka kwa viwango vya halijoto na mabadiliko ya tabianchi limeibua mijadala ya kitaifa na kimataifa. Kwa msingi huu, kazi mbalimbali za kifasihi zimebuniwa kwa kuangazia uharibifu wa mazingira asilia na athari zake na mwito wa kuhifadhi mazingira. Makala hii ilikusudia kuchunguza jinsi motifu za kimazingira zilivyosawiriwa katika tamthilia ya Majira ya Utasa (Arege, 2015). Msisitizo ulikuwa kuangazia jinsi mwandishi wa tamthilia teule amesawiri motifu za kimazingira ili kuonyesha uharibifu wa mazingira pamoja na matatizo yanayotokana na uharibifu huo. Hii ni kwa sababu fasihi huwasilisha hali, maingiliano na mikinzano miongoni mwa binadamu na mazingira. Kwa hivyo, ni mojawapo ya nyenzo inayoweza kuchangia katika kuangazia matatizo yanayokumba jamii yoyote iwayo. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia iliyoasisiwa na Glotferty (1996). Kimsingi, nadharia ya uhakiki wa kiekolojia hujikita katika uchambuzi wa kazi za kifasihi kwa kuonyesha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Tamthilia iliyohakikiwa iliteuliwa kimakusudi kwa kuwa maudhui yake makuu yanahusiana moja kwa moja na mada ya makala hii. Ukusanyaji wa data ulifanywa kupitia usomaji wa kina wa tamthilia teule. Matokeo ya makala hii yalithibitisha kuwa mwandishi wa tamthilia ya Majira ya Utasa amesawiri motifu za kimazingira kwa namna mbalimbali kwa kuonyesha njia za uharibifu wa mazingira na athari zake. Hivyo, kushadidia kuwa fasihi inaakisi kikamilifu matatizo yanayoibuka katika jamii ilimoibuka. Kwa hivyo, ni chombo madhubuti kinachoweza kutumiwa kutatua matatizo hayo.