{"title":"Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma","authors":"Martin Barasa Mulwale, F. Indede, B. Ambuyo","doi":"10.37284/jammk.6.1.1147","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufahamu na kutagusana na ulimwengu huhitaji matumizi ya kiisimu ya kipekee. Katika muktadha wa kidini kuna changamoto ya asili ya maneno, mamlaka, utambulisho na ushirikiano wa wahusika. Aidha, miktadha mbalimbali ya kidini hutumia lugha kutimiza mahitaji yake maalum. Lugha hutenda matendo, huomba maombi ya kukemea, husimulia hali za kijamii na hata huonekana kudhibiti matendo ya Maulana. Ni kwa misingi hii ndipo kazi hii inajukumika kutalii jinsi lugha ya Kiswahili na Kibukusu zinavyotagusana katika mawanda haya ya dini, hasa Dini ya Musambwa (DYM) ambayo inaaminika kuwa ya kiasili katika jamii hii ya Wabukusu katika Kaunti ya Bungoma. Kazi hii inazingatia misingi ya Spolsky (2004, 2006, 2009) ambaye anajadili kuwa sera ya lugha halisi ya jamii hupatikana kwenye matumizi yake. Anazingatia Mwelekeo wa ikolojia ya lugha uliozinduliwa na Haugen (1972) unaochunguza mwingiliano baina ya lugha na mazingira. Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa. Kupitia uchunzaji wa kutoshiriki moja kwa moja mtafiti alihudhuria ibada na kunasa mazungumzo yao kwenye kanda ya kunasia sauti. Mazungumzo hayo yalinakiliwa na orodha ya uchunzaji ilitumiwa kubainisha na kueleza namna lugha ya Kibukusu na Kiswahili zilivyotumiwa katika shughuli za kanisa hilo. Hali ya kuchanganya na kubadili msimbo, utohozi na hata matumizi ya Kiswahili kwa Kibukusu haikuweza kuepukika. Utafiti huu unadhihirisha kuwa raslimali za lugha zilizopo katika ikolojia fulani huchagizana katika kukamilisha majukumu ya mawasiliano katika muktadha husika.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-03-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1147","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufahamu na kutagusana na ulimwengu huhitaji matumizi ya kiisimu ya kipekee. Katika muktadha wa kidini kuna changamoto ya asili ya maneno, mamlaka, utambulisho na ushirikiano wa wahusika. Aidha, miktadha mbalimbali ya kidini hutumia lugha kutimiza mahitaji yake maalum. Lugha hutenda matendo, huomba maombi ya kukemea, husimulia hali za kijamii na hata huonekana kudhibiti matendo ya Maulana. Ni kwa misingi hii ndipo kazi hii inajukumika kutalii jinsi lugha ya Kiswahili na Kibukusu zinavyotagusana katika mawanda haya ya dini, hasa Dini ya Musambwa (DYM) ambayo inaaminika kuwa ya kiasili katika jamii hii ya Wabukusu katika Kaunti ya Bungoma. Kazi hii inazingatia misingi ya Spolsky (2004, 2006, 2009) ambaye anajadili kuwa sera ya lugha halisi ya jamii hupatikana kwenye matumizi yake. Anazingatia Mwelekeo wa ikolojia ya lugha uliozinduliwa na Haugen (1972) unaochunguza mwingiliano baina ya lugha na mazingira. Muundo wa kiuchanganuzi ulitumiwa. Kupitia uchunzaji wa kutoshiriki moja kwa moja mtafiti alihudhuria ibada na kunasa mazungumzo yao kwenye kanda ya kunasia sauti. Mazungumzo hayo yalinakiliwa na orodha ya uchunzaji ilitumiwa kubainisha na kueleza namna lugha ya Kibukusu na Kiswahili zilivyotumiwa katika shughuli za kanisa hilo. Hali ya kuchanganya na kubadili msimbo, utohozi na hata matumizi ya Kiswahili kwa Kibukusu haikuweza kuepukika. Utafiti huu unadhihirisha kuwa raslimali za lugha zilizopo katika ikolojia fulani huchagizana katika kukamilisha majukumu ya mawasiliano katika muktadha husika.