{"title":"Muwala katika Vikatuni vya Shujaaz: Mtazamo wa Kiuchanganuzi Makinifu wa Diskosi","authors":"Dimbu Sammy Liana, John M. Kobia, Allan Mugambi","doi":"10.37284/jammk.5.1.759","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Vikatuni vina wajibu muhimu katika aushi ya vijana ulimwenguni. Huenda ndio sababu Karne ya 21 imeshuhudia ongezeko la tafiti kuhusu vikatuni. Kumekuwepo na tafiti nyingi kuhusu muwala katika uwanja wa kiusomi. Tafiti za awali zilijikita kwenye muwala katika makala, magazeti, tasnifu, vitabu na vikatuni. Hata hivyo, hakuna utafiti kuhusu muwala katika vikatuni wa Shujaaz. Makala hii inalenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kueleza namna muwala ulivyokuzwa katika diskosi ya vikatuni vya Shujaaz. Diskosi hii ni jarida linalowasilishwa kupitia msimbo wa Sheng ambalo hulenga vijana kuanzia umri wa miaka 12 hadi 35. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Mojawapo wa madhumuni ya nadharia hii ni kusaidia katika uchanganuzi wa diskosi ili kufichua imani za kiitikadi zinazochukuliwa kuwa za ukweli na kukubaliwa katika jamii. Data ya makala hii ilitokana na sampuli ya nakala 35 zilizoteuliwa kimakusudi kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Matokeo ni kuwa muwala hukuzwa kupitia: mada, sauti za kionomatopeya, maandishi panelini na maelezo ya mwandishi. Aina ya muwala uliokuzwa ulitokana na msuko wa hadithi, muwala wa jumla na mada. Utafiti huu unaweka wazi namna kampuni ya WellTold Story ilivyotumia maarifa ya kiusuli katika jamii kukuza muwala wa jumla kama mkakati wa kuendeleza na kuwawekea vijana vizingiti ili kuwadhibiti. Hivyo serikali na mashirika ya kijamii yanaweza kutumia mkakati huu katika kuwaelimisha vijana kuhusu magonjwa ya majanga makubwa kama njia moja ya kupunguza athari zake kwa jamii.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"11 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-07-19","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.759","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Vikatuni vina wajibu muhimu katika aushi ya vijana ulimwenguni. Huenda ndio sababu Karne ya 21 imeshuhudia ongezeko la tafiti kuhusu vikatuni. Kumekuwepo na tafiti nyingi kuhusu muwala katika uwanja wa kiusomi. Tafiti za awali zilijikita kwenye muwala katika makala, magazeti, tasnifu, vitabu na vikatuni. Hata hivyo, hakuna utafiti kuhusu muwala katika vikatuni wa Shujaaz. Makala hii inalenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kueleza namna muwala ulivyokuzwa katika diskosi ya vikatuni vya Shujaaz. Diskosi hii ni jarida linalowasilishwa kupitia msimbo wa Sheng ambalo hulenga vijana kuanzia umri wa miaka 12 hadi 35. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makinifu wa Diskosi. Mojawapo wa madhumuni ya nadharia hii ni kusaidia katika uchanganuzi wa diskosi ili kufichua imani za kiitikadi zinazochukuliwa kuwa za ukweli na kukubaliwa katika jamii. Data ya makala hii ilitokana na sampuli ya nakala 35 zilizoteuliwa kimakusudi kwa kuzingatia kigezo cha yaliyomo. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Matokeo ni kuwa muwala hukuzwa kupitia: mada, sauti za kionomatopeya, maandishi panelini na maelezo ya mwandishi. Aina ya muwala uliokuzwa ulitokana na msuko wa hadithi, muwala wa jumla na mada. Utafiti huu unaweka wazi namna kampuni ya WellTold Story ilivyotumia maarifa ya kiusuli katika jamii kukuza muwala wa jumla kama mkakati wa kuendeleza na kuwawekea vijana vizingiti ili kuwadhibiti. Hivyo serikali na mashirika ya kijamii yanaweza kutumia mkakati huu katika kuwaelimisha vijana kuhusu magonjwa ya majanga makubwa kama njia moja ya kupunguza athari zake kwa jamii.