{"title":"Utekelezaji wa Mitalaa ya Kiswahili Vyuoni na Namna Unavyoathiri Utendakazi wa Walimu Wanaofundisha katika Shule za Upili","authors":"Jackline Mwanzi, Odeo Isaac Ipara, K. I. Simala","doi":"10.37284/jammk.5.1.556","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Walimu wanaofundisha katika shule za upili hupata mafunzo yao ya kitaaluma kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali. Wanapoandaliwa vyuoni, walimu hawa hupewa mafunzo kwa kutumia mitalaa tofauti inayoandaliwa katika vyuo vikuu hivyo. Baada ya kuhitimu, wao hutarajiwa kuutekeleza mtalaa mmoja unaoandaliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitalaa nchini Kenya (TUMIKE) ili ufundishwe katika shule zote za upili. Utafiti ulifanywa ili kudhihirisha iwapo mafunzo ya kitaaluma yanayotolewa vyuoni kuwaandaa walimu wa somo la Kiswahili yanawapa maarifa na stadi wanazohitaji kufundisha katika shule za upili baada ya kuhitimu. Makala haya yametokana na utafiti uliofanywa ili Kutathmini uhusiano baina ya mitalaa ya Kiswahili inayotumika katika vyuo vikuu vya umma nchini Kenya na mtalaa ambao umeandaliwa na TUMIKE ili kutekelezwa katika shule za upili. Utafiti ulifanyika katika vyuo vikuu vitano vya umma nchini Kenya. Muundo wa utafiti ulikuwa usoroveya elezi. Data ilikusanywa kwa njia ya usaili, uchanganuzi wa nyaraka na hojaji. Uchanganuzi wa data ulikuwa wa kitakwimu na kimaelezo. Utafiti uligundua kuwa uhusiano baina ya mitalaa rasmi ya Kiswahili ya vyuo vikuu vya umma na mtalaa wa Kiswahili wa shule za upili siyo wa moja kwa moja. Hali hii iliathiri utendakazi wa walimu walipotekeleza mtalaa wa shule za upili. Uhusiano mdogo uliopo baina ya mitalaa rasmi ya vyuo vikuu na mtalaa rasmi wa TUMIKE ulidhihirika kwa kuchunguza vipengele vikuu vya mtalaa ambavyo ni: malengo, mada, utekelezaji na tathmini. Utafiti unapendekeza pafanyike marekebisho ya mara kwa mara ya mtalaa wa TUMIKE kwa kuwahusisha walimu na waandalizi wao ili wakadirie malengo, mada, mbinu za utekelezaji na tathmini mintarafu maandalizi yanayotolewa kwa walimu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-02-18","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.556","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Walimu wanaofundisha katika shule za upili hupata mafunzo yao ya kitaaluma kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali. Wanapoandaliwa vyuoni, walimu hawa hupewa mafunzo kwa kutumia mitalaa tofauti inayoandaliwa katika vyuo vikuu hivyo. Baada ya kuhitimu, wao hutarajiwa kuutekeleza mtalaa mmoja unaoandaliwa na Taasisi ya Ukuzaji Mitalaa nchini Kenya (TUMIKE) ili ufundishwe katika shule zote za upili. Utafiti ulifanywa ili kudhihirisha iwapo mafunzo ya kitaaluma yanayotolewa vyuoni kuwaandaa walimu wa somo la Kiswahili yanawapa maarifa na stadi wanazohitaji kufundisha katika shule za upili baada ya kuhitimu. Makala haya yametokana na utafiti uliofanywa ili Kutathmini uhusiano baina ya mitalaa ya Kiswahili inayotumika katika vyuo vikuu vya umma nchini Kenya na mtalaa ambao umeandaliwa na TUMIKE ili kutekelezwa katika shule za upili. Utafiti ulifanyika katika vyuo vikuu vitano vya umma nchini Kenya. Muundo wa utafiti ulikuwa usoroveya elezi. Data ilikusanywa kwa njia ya usaili, uchanganuzi wa nyaraka na hojaji. Uchanganuzi wa data ulikuwa wa kitakwimu na kimaelezo. Utafiti uligundua kuwa uhusiano baina ya mitalaa rasmi ya Kiswahili ya vyuo vikuu vya umma na mtalaa wa Kiswahili wa shule za upili siyo wa moja kwa moja. Hali hii iliathiri utendakazi wa walimu walipotekeleza mtalaa wa shule za upili. Uhusiano mdogo uliopo baina ya mitalaa rasmi ya vyuo vikuu na mtalaa rasmi wa TUMIKE ulidhihirika kwa kuchunguza vipengele vikuu vya mtalaa ambavyo ni: malengo, mada, utekelezaji na tathmini. Utafiti unapendekeza pafanyike marekebisho ya mara kwa mara ya mtalaa wa TUMIKE kwa kuwahusisha walimu na waandalizi wao ili wakadirie malengo, mada, mbinu za utekelezaji na tathmini mintarafu maandalizi yanayotolewa kwa walimu.