Melvin Atieno Ouma, Jonathan Furaha Chai, C. Kitetu
{"title":"‘Huyu Mtu Hasimami’: Uhuishi katika Mazungumzo ya Daktari na Wanaume katika Kliniki ya Afya ya Uzazi, Kenya","authors":"Melvin Atieno Ouma, Jonathan Furaha Chai, C. Kitetu","doi":"10.37284/jammk.5.1.685","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Lugha ni kiungo muhimu katika mawasiliano kati ya daktari na mgonjwa. Katika kliniki ya afya ya uzazi, kutaja sehemu za mwili kwa majina yao ni kigezo muhimu katika utoaji na upokeaji wa huduma za afya. Ujinaishaji ni jambo la zamani kama ilivyo ubinadamu. Ujinaishaji wa sehemu za siri ina historia ndefu kutoka karne ya zamani sana. Ujinaishaji wa sehemu hizi ni jambo linalofanyika katika mataifa yote ulimwenguni. Makala haya yanaangazia uhuishi unavyotumiwa na wanaume kama mkakati wa mazungumzo katika kliniki ya afya ya uzazi. Kuafikia hili, makala haya yatashughulikia majina ambayo wanaume wanayapa sehemu zao za siri katika kliniki ya afya ya uzazi. Pia yatafafanua sifa na tabia za kibinadamu zinazopewa sehemu za siri katika mazungumzo ya wanaume na daktari kuhusu matatizo ya afya ya uzazi. Majina kama vile dick, mwanaume, uume, mkuki, chuma na huyu mtu ni baadhi ya majina wanaume walitumia kutaja sehemu zao za siri. Sehemu za siri ya wanaume ilipewa sifa na tabia za kibinadamu kupitia urejeleo kwa ngeli ya A-WA. Matumizi ya ngeli ya A-WA ni idhibati kuwa dhakari ni kama binadamu na wala si sehemu ya mwili ya kawaida kama inavyodhaniwa. Uhuishi ulijitokeza katika mazungumzo kupitia maneno kama vile anakataa, hakubali, hasimami, anajikunja. Semi za wanaume zinaonyesha kuwa dhakari ina uwezo wa kuamuka na kufanya kazi. Dhakari ina uwezo wa kutoa adhabu. Ina uwezo wa kusimama. Ina uwezo wa kuwa imara na ina uwezo wa kuenda. Sehemu za siri za mwanamume zina maisha yake na fahamu zake kando na yule mwanamume anayemiliki sehemu hizo. Kupitia mazungumzo ya daktari na mgonjwa, sehemu za siri (dhakari) ndio sehemu ya mwili inayothaminiwa zaidi miongoni mwa wanaume.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"89 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-05-30","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.685","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Lugha ni kiungo muhimu katika mawasiliano kati ya daktari na mgonjwa. Katika kliniki ya afya ya uzazi, kutaja sehemu za mwili kwa majina yao ni kigezo muhimu katika utoaji na upokeaji wa huduma za afya. Ujinaishaji ni jambo la zamani kama ilivyo ubinadamu. Ujinaishaji wa sehemu za siri ina historia ndefu kutoka karne ya zamani sana. Ujinaishaji wa sehemu hizi ni jambo linalofanyika katika mataifa yote ulimwenguni. Makala haya yanaangazia uhuishi unavyotumiwa na wanaume kama mkakati wa mazungumzo katika kliniki ya afya ya uzazi. Kuafikia hili, makala haya yatashughulikia majina ambayo wanaume wanayapa sehemu zao za siri katika kliniki ya afya ya uzazi. Pia yatafafanua sifa na tabia za kibinadamu zinazopewa sehemu za siri katika mazungumzo ya wanaume na daktari kuhusu matatizo ya afya ya uzazi. Majina kama vile dick, mwanaume, uume, mkuki, chuma na huyu mtu ni baadhi ya majina wanaume walitumia kutaja sehemu zao za siri. Sehemu za siri ya wanaume ilipewa sifa na tabia za kibinadamu kupitia urejeleo kwa ngeli ya A-WA. Matumizi ya ngeli ya A-WA ni idhibati kuwa dhakari ni kama binadamu na wala si sehemu ya mwili ya kawaida kama inavyodhaniwa. Uhuishi ulijitokeza katika mazungumzo kupitia maneno kama vile anakataa, hakubali, hasimami, anajikunja. Semi za wanaume zinaonyesha kuwa dhakari ina uwezo wa kuamuka na kufanya kazi. Dhakari ina uwezo wa kutoa adhabu. Ina uwezo wa kusimama. Ina uwezo wa kuwa imara na ina uwezo wa kuenda. Sehemu za siri za mwanamume zina maisha yake na fahamu zake kando na yule mwanamume anayemiliki sehemu hizo. Kupitia mazungumzo ya daktari na mgonjwa, sehemu za siri (dhakari) ndio sehemu ya mwili inayothaminiwa zaidi miongoni mwa wanaume.