{"title":"Mchango wa Kiswahili katika Mofofonolojia ya Nominomkopo za Lubukusu","authors":"Tom Juma James, Jacktone O. Onyango","doi":"10.37284/jammk.6.1.1162","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Ukopaji wa leksimu baina ya lugha tofauti ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Kwa hivyo, makala haya yamechunguza jinsi lugha ya Kiswahili imechangia katika upanuzi wa Lubukusu kimofofonolojia kupitia ukopaji wa nomino. Hali hii ilisababishwa na dhana kwamba Kiswahili kimeathiri Lubukusu kiisimu kupitia vipengele kama vile fonolojia, mofolojia na sintaksia. Hata hivyo,makala haya yamejikita tu katika viwango viwili vya kiisimu; fonolojia na mofolojia. Malengo matatu yalishughulikiwa katika makala haya ambayo ni: kubainisha mabadiliko ya kifonolojia yaliyojitokeza katika nominomkopo kutoka Kiswahili hadi Lubukusu, kutambulisha mabadiliko ya kimofolojia yaliyojitokeza katika nominomkopo kutoka Kiswahili hadi Lubukusu na kuchunguza ulinganifu wa kifonolojia na kimofolojia uliopo baina ya nominomkopo za Lubukusu na leksimu changizi za Kiswahili. Hatua zote za makala haya zilitimizwa kupitia mihimili ya nadharia ya Mlingano Chanzi, modeli ya kiutohozi iliyoasisiwa na Smith (2009) na ni maendelezo ya Nadharia Upeo (OptimalityTheory) iliyopendekezwa na Prince na Smolensky (1993). Data ilikusanywa kutoka maktabani na nyanjani. Data ya maktabani ilipatikana kupitia udurusu wa vitabu, tasnifu, majarida na makala ya mtandaoni. Nyanjani, sampuli iliteuliwa kimaksudi kupitia mahojiano kwa walengwa 24 wa jamiilugha ya Babukusu kutoka Kaunti Ndogo ya Kiminini, Kauntiya Trans-Nzoia. Mahojiano yalihusu habari za kibinafsi na maswali teule kutoka kwa vikoa 12 vya kisemantiki. Uchanganuzi wa nominomkopo zilizokusanywa kutoka nyanjani ulidhihirisha kwamba kuna mfanano wa kimaumbo kati ya nomino hizo zikiwa katika mazingiraya Kiswahili na hata zinapohamishiwa katika mazingira ya Lubukusu. Uchunguzi wa matokeo ulionyesha kwamba nominokopwa za Lubukusu kutoka Kiswahili hupitia mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia na mabadiliko hayo yaliongozwa na sheria za kimofofonolojia zilizorahisisha usimilisho wa nomino hizo kopwa katika sarufi ya Lubukusu. \n ","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"43 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-04-06","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1162","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Ukopaji wa leksimu baina ya lugha tofauti ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Kwa hivyo, makala haya yamechunguza jinsi lugha ya Kiswahili imechangia katika upanuzi wa Lubukusu kimofofonolojia kupitia ukopaji wa nomino. Hali hii ilisababishwa na dhana kwamba Kiswahili kimeathiri Lubukusu kiisimu kupitia vipengele kama vile fonolojia, mofolojia na sintaksia. Hata hivyo,makala haya yamejikita tu katika viwango viwili vya kiisimu; fonolojia na mofolojia. Malengo matatu yalishughulikiwa katika makala haya ambayo ni: kubainisha mabadiliko ya kifonolojia yaliyojitokeza katika nominomkopo kutoka Kiswahili hadi Lubukusu, kutambulisha mabadiliko ya kimofolojia yaliyojitokeza katika nominomkopo kutoka Kiswahili hadi Lubukusu na kuchunguza ulinganifu wa kifonolojia na kimofolojia uliopo baina ya nominomkopo za Lubukusu na leksimu changizi za Kiswahili. Hatua zote za makala haya zilitimizwa kupitia mihimili ya nadharia ya Mlingano Chanzi, modeli ya kiutohozi iliyoasisiwa na Smith (2009) na ni maendelezo ya Nadharia Upeo (OptimalityTheory) iliyopendekezwa na Prince na Smolensky (1993). Data ilikusanywa kutoka maktabani na nyanjani. Data ya maktabani ilipatikana kupitia udurusu wa vitabu, tasnifu, majarida na makala ya mtandaoni. Nyanjani, sampuli iliteuliwa kimaksudi kupitia mahojiano kwa walengwa 24 wa jamiilugha ya Babukusu kutoka Kaunti Ndogo ya Kiminini, Kauntiya Trans-Nzoia. Mahojiano yalihusu habari za kibinafsi na maswali teule kutoka kwa vikoa 12 vya kisemantiki. Uchanganuzi wa nominomkopo zilizokusanywa kutoka nyanjani ulidhihirisha kwamba kuna mfanano wa kimaumbo kati ya nomino hizo zikiwa katika mazingiraya Kiswahili na hata zinapohamishiwa katika mazingira ya Lubukusu. Uchunguzi wa matokeo ulionyesha kwamba nominokopwa za Lubukusu kutoka Kiswahili hupitia mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia na mabadiliko hayo yaliongozwa na sheria za kimofofonolojia zilizorahisisha usimilisho wa nomino hizo kopwa katika sarufi ya Lubukusu.