{"title":"Dhima za Tasifida Kimuktadha katika Nyimbo za Singeli: Mifano kutoka kwa Msanii Msaga Sumu na Manfongo","authors":"Baraka Sikuomba, Lina Godfrey","doi":"10.37284/jammk.6.1.1470","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Kutokana na ufinyu wa tafiti zilizofanyika kuhusu tasifida katika muktadha wa nyimbo za singeli kumejengeka mtazamo hasi hasa kwenye lugha inayotumika katika muktadha wa nyimbo za singeli miongoni mwa wanajamii. Kutokana na umuhimu wa tasifida katika kuendeleza utamaduni wa jamii kulikuwa na haja ya kuchunguza na kuweka bayana dhima za matumizi ya tasifida katika nyimbo za singeli. Kwa hiyo, makala hii imeangalia dhima za tasifida kimuktadha katika nyimbo za singeli kwa kutumia nyimbo ziitwazo “Siponaye”, “Dada Asha”, “Spesho”, “Mtoto Mdogo” za msanii Msaga Sumu na “Chawa”, “Hainogi”, “Kitasa”, “Mashine” “Kipusa”, “Muacheni Adange” za msanii Manfongo. Nadharia ya Semiotiki imetumika kufafanua dhima za tasifida katika nyimbo za wasanii teule. Katika nyimbo hizo tasifida mbalimbali zimetumiwa na wasanii teule kuwasilisha maudhui yao. Nyimbo hizi za singeli, licha ya kuimbwa kwa lugha inayoonekana ni ya mtaani, zimezingatia sana matumizi ya tasifida katika kupunguza ukali wa maneno. Matokeo ya utafiti huu yameonesha wazi kuwa matumizi ya lugha ya tasifida katika nyimbo za singeli, yameonesha wazi kwamba nyimbo za singeli zina dhima kadha wa kadha zinazowasilishwa kwa njia ya matumizi ya tasifida. Kupitia matumizi ya tasifida katika nyimbo za singeli, ni bayana kwamba tasifida zina dhima za msingi katika nyimbo za singeli katika kuendeleza mila, utamaduni na desturi za mawasiliano katika jamii. Dhima hizo ni pamoja na kubainisha kazi zisizo halali katika jamii, kuibua tabia zisizokubarika katika jamii, kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii, kuhimiza umuhimu wa mapenzi ya dhati katika jamii na kuweka bayana uhalisia wa mwanaume. Hivyo basi, watafiti wengine wanaweza kufanya utafiti kama huu kwa kuchunguza kwa kina tofauti ya tasifida na taswira kimuktadha katika nyimbo teule za utafiti huu","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"52 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2023-09-27","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African Journal of Swahili Studies","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1470","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Kutokana na ufinyu wa tafiti zilizofanyika kuhusu tasifida katika muktadha wa nyimbo za singeli kumejengeka mtazamo hasi hasa kwenye lugha inayotumika katika muktadha wa nyimbo za singeli miongoni mwa wanajamii. Kutokana na umuhimu wa tasifida katika kuendeleza utamaduni wa jamii kulikuwa na haja ya kuchunguza na kuweka bayana dhima za matumizi ya tasifida katika nyimbo za singeli. Kwa hiyo, makala hii imeangalia dhima za tasifida kimuktadha katika nyimbo za singeli kwa kutumia nyimbo ziitwazo “Siponaye”, “Dada Asha”, “Spesho”, “Mtoto Mdogo” za msanii Msaga Sumu na “Chawa”, “Hainogi”, “Kitasa”, “Mashine” “Kipusa”, “Muacheni Adange” za msanii Manfongo. Nadharia ya Semiotiki imetumika kufafanua dhima za tasifida katika nyimbo za wasanii teule. Katika nyimbo hizo tasifida mbalimbali zimetumiwa na wasanii teule kuwasilisha maudhui yao. Nyimbo hizi za singeli, licha ya kuimbwa kwa lugha inayoonekana ni ya mtaani, zimezingatia sana matumizi ya tasifida katika kupunguza ukali wa maneno. Matokeo ya utafiti huu yameonesha wazi kuwa matumizi ya lugha ya tasifida katika nyimbo za singeli, yameonesha wazi kwamba nyimbo za singeli zina dhima kadha wa kadha zinazowasilishwa kwa njia ya matumizi ya tasifida. Kupitia matumizi ya tasifida katika nyimbo za singeli, ni bayana kwamba tasifida zina dhima za msingi katika nyimbo za singeli katika kuendeleza mila, utamaduni na desturi za mawasiliano katika jamii. Dhima hizo ni pamoja na kubainisha kazi zisizo halali katika jamii, kuibua tabia zisizokubarika katika jamii, kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii, kuhimiza umuhimu wa mapenzi ya dhati katika jamii na kuweka bayana uhalisia wa mwanaume. Hivyo basi, watafiti wengine wanaweza kufanya utafiti kama huu kwa kuchunguza kwa kina tofauti ya tasifida na taswira kimuktadha katika nyimbo teule za utafiti huu