{"title":"VYANZO VYA MISIMU KWA WANAFUNZI KATIKA KISWAHILI","authors":"Editha Adolph","doi":"10.58721/jkal.v1i1.92","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Makala hii inachunguza vyanzo vya misimu kwa wanafunzi katika Kiswahili. Mtafiti ametumia mbinu za hojaji, usaili na uchambuzi wa matini. Mtafiti aligawa hojaji 15 kwa wanachuo 15 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Chuo hiki kinapatikana katika Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam nchini Tanzania. Aidha, mtafiti alisoma nyaraka zinazohusiana na mada husika kama vile: majarida na tasinifu. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi wa Kimaeneo ya Fishman (1972). Data ya makala hii imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa maelezo. Matokeo ya makala hii yamebainisha kuwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na kutumia msamiati sanifu pia hutumia misimu kutoka katika nyanja tofautitofauti katika mawasiliano yao ya kila siku. Mtafiti amechunguza misimu inayotokana na uwanja wa sanaa, siasa na michezo. Makala hii ni muhimu kwa wanaisimu kwani inabainisha misimu mbalimbali inayotumiwa na wanachuo wa chuo husika. Pia misimu tofautitofauti inayohusiana na nyanja za utani, soka na sanaa. Hii itatoa msukumo kwa wasanifishaji wa lugha ya Kiswahili kusanifisha misimu husika. Makala inapendekeza kuwa watafiti wa lugha wachunguze misimu inayotokana na mitandao ya kijamii, aina mbalimbali za misimu, misimu inayotumika katika maeneo mbalimbali kama vile shuleni, vijiweni, hospitalini na maofini.","PeriodicalId":433758,"journal":{"name":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","volume":"51 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2022-11-28","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"Journal of Kiswahili and Other African Languages","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.58721/jkal.v1i1.92","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Makala hii inachunguza vyanzo vya misimu kwa wanafunzi katika Kiswahili. Mtafiti ametumia mbinu za hojaji, usaili na uchambuzi wa matini. Mtafiti aligawa hojaji 15 kwa wanachuo 15 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Chuo hiki kinapatikana katika Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam nchini Tanzania. Aidha, mtafiti alisoma nyaraka zinazohusiana na mada husika kama vile: majarida na tasinifu. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi wa Kimaeneo ya Fishman (1972). Data ya makala hii imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa maelezo. Matokeo ya makala hii yamebainisha kuwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na kutumia msamiati sanifu pia hutumia misimu kutoka katika nyanja tofautitofauti katika mawasiliano yao ya kila siku. Mtafiti amechunguza misimu inayotokana na uwanja wa sanaa, siasa na michezo. Makala hii ni muhimu kwa wanaisimu kwani inabainisha misimu mbalimbali inayotumiwa na wanachuo wa chuo husika. Pia misimu tofautitofauti inayohusiana na nyanja za utani, soka na sanaa. Hii itatoa msukumo kwa wasanifishaji wa lugha ya Kiswahili kusanifisha misimu husika. Makala inapendekeza kuwa watafiti wa lugha wachunguze misimu inayotokana na mitandao ya kijamii, aina mbalimbali za misimu, misimu inayotumika katika maeneo mbalimbali kama vile shuleni, vijiweni, hospitalini na maofini.