{"title":"Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia","authors":"Nanjala Nyabola","doi":"10.1108/fs-11-2021-0222","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"\nPurpose\nManeno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidijitali hutumia maneno ya Kiingereza – hata bila utohozi – wanapozungumzia haki za kiteknolojia. Hali hii ya mambo inachangia udhoofu fulani katika utetezi wa haki za kidijitali kwani wanaojaribu kueleza jamii umuhimu wa haki hizi hulazimishwa kutegemea msamiati wa Kiingereza usiyo na msingi au viungo na lugha ya Kiswahili Katika makala hii, tutazungumzia umuhimu wa kukaribisha watu kutumia lugha za Kiafrika kwenye mtandao.\n\n\nDesign/methodology/approach\nKiswahili ni lugha ya Kiafrika inayozungumzwa katika eneo zaidi sana duniani. Karibu watu milioni mia moja na arobaini Afrika mashariki wanazungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza au ya pili, miongoni mwao Wakenya na Watanzania, wenyeji wa nchi ambamo Kiswahili ni lugha ya kitaifa. Tena kuna historia ndefu ya kutumiwa kwa lugha ya Kiswahili katika uandishi, uchapishaji na ubunifu wa utamaduni wa kisasa. Kiswahili pekee yake ndiyo lugha ya asili ya Kiafrika inayotumika kama lugha ya maalum ya Umoja wa Mataifa za Kiafrika. Hata hivyo, kwa upande wa matumizi ya Kiswahili, hasa kwenye mada ya teknolojia, Kiswahili imewachwa nyuma.\n\n\nFindings\nZaidi ya maneno rasmi, uwepo wa lugha za Kiafrika ni muhimu kuimarisha jumuiya za Kiafrika mtandaoni kwani lugha inalenga sana haki na utambulisho wa watu. Miradi za kutafsiri maneno za kiteknolojia katika lugha ya Kiswahili inahimiza jumuiya za Afrika Mashariki kuunda jamii inayosimamia matakwa yao vyema. Makala hii basi inazingatia umuhimu wa lugha kwenye kuunda jamii na katika hatua za kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni ili wenyeji wa Afrika Mashariki wajione mtandaoni kwa ujumla wao wote. Makala pia itazingatia semiotiki ya lugha katika ubunifu wa teknolojia, na umuhimu wa kutafsiri jamii ya lugha ya Kiswahili katika harakati za kuondoa ukoloni katika ubunifu huu. Lakini sio tu kwamba lugha ya Kiswahili ndio pekee inayoweza kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni, kwani pia lugha hiyo ina ishara za kutawalwa kwa jamii fulani. Bali makala hii inatumia mfano wa Kiswahili kuhimiza utumiaji wa lugha za kiasili au za kimama mtandaoni ili kulinda mustakabali wa kidijitali wa umma.\n\n\nOriginality/value\nUmuhimu wa makala hii ni kuashiria jipya umuhimu wa lugha katika harakati za kuendeleza haki za kidijitali na hasa kuondoa mbinu za kikoloni kwenye teknolojia, swala lisilowahijadiliwa katika lugha ya Kiswahili.\n","PeriodicalId":51620,"journal":{"name":"Foresight","volume":" ","pages":""},"PeriodicalIF":2.3000,"publicationDate":"2022-10-13","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"Foresight","FirstCategoryId":"1085","ListUrlMain":"https://doi.org/10.1108/fs-11-2021-0222","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"Q3","JCRName":"REGIONAL & URBAN PLANNING","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidijitali hutumia maneno ya Kiingereza – hata bila utohozi – wanapozungumzia haki za kiteknolojia. Hali hii ya mambo inachangia udhoofu fulani katika utetezi wa haki za kidijitali kwani wanaojaribu kueleza jamii umuhimu wa haki hizi hulazimishwa kutegemea msamiati wa Kiingereza usiyo na msingi au viungo na lugha ya Kiswahili Katika makala hii, tutazungumzia umuhimu wa kukaribisha watu kutumia lugha za Kiafrika kwenye mtandao.
Design/methodology/approach
Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayozungumzwa katika eneo zaidi sana duniani. Karibu watu milioni mia moja na arobaini Afrika mashariki wanazungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza au ya pili, miongoni mwao Wakenya na Watanzania, wenyeji wa nchi ambamo Kiswahili ni lugha ya kitaifa. Tena kuna historia ndefu ya kutumiwa kwa lugha ya Kiswahili katika uandishi, uchapishaji na ubunifu wa utamaduni wa kisasa. Kiswahili pekee yake ndiyo lugha ya asili ya Kiafrika inayotumika kama lugha ya maalum ya Umoja wa Mataifa za Kiafrika. Hata hivyo, kwa upande wa matumizi ya Kiswahili, hasa kwenye mada ya teknolojia, Kiswahili imewachwa nyuma.
Findings
Zaidi ya maneno rasmi, uwepo wa lugha za Kiafrika ni muhimu kuimarisha jumuiya za Kiafrika mtandaoni kwani lugha inalenga sana haki na utambulisho wa watu. Miradi za kutafsiri maneno za kiteknolojia katika lugha ya Kiswahili inahimiza jumuiya za Afrika Mashariki kuunda jamii inayosimamia matakwa yao vyema. Makala hii basi inazingatia umuhimu wa lugha kwenye kuunda jamii na katika hatua za kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni ili wenyeji wa Afrika Mashariki wajione mtandaoni kwa ujumla wao wote. Makala pia itazingatia semiotiki ya lugha katika ubunifu wa teknolojia, na umuhimu wa kutafsiri jamii ya lugha ya Kiswahili katika harakati za kuondoa ukoloni katika ubunifu huu. Lakini sio tu kwamba lugha ya Kiswahili ndio pekee inayoweza kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni, kwani pia lugha hiyo ina ishara za kutawalwa kwa jamii fulani. Bali makala hii inatumia mfano wa Kiswahili kuhimiza utumiaji wa lugha za kiasili au za kimama mtandaoni ili kulinda mustakabali wa kidijitali wa umma.
Originality/value
Umuhimu wa makala hii ni kuashiria jipya umuhimu wa lugha katika harakati za kuendeleza haki za kidijitali na hasa kuondoa mbinu za kikoloni kwenye teknolojia, swala lisilowahijadiliwa katika lugha ya Kiswahili.
期刊介绍:
■Social, political and economic science ■Sustainable development ■Horizon scanning ■Scientific and Technological Change and its implications for society and policy ■Management of Uncertainty, Complexity and Risk ■Foresight methodology, tools and techniques