{"title":"Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado","authors":"Kerryann Wanjiku Mburu, Sheila Wandera-Simwa, Nabea Wendo","doi":"10.37284/jammk.7.1.1685","DOIUrl":null,"url":null,"abstract":"Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizoweza kusemwa wazi wazi. Ifahamike kuwa sifa kuu ya vibonzo vya kisiasa ni kuwa vinapaswa kuwa cheshi na vyenye tashtiti ndiposa viweze kuwasilisha masuala tata kwa njia ya kimzaha. Kutokana na hali hii, utafiti huu ulichunguza tashtiti katika vibonzo vya kisiasa vya Gado vilivyochapishwa katika mwaka wa 2017 kwenye tovuti yake. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kupambanua mikakati iliyotumika katika kuendeleza maudhui ya kitashtiti katika vibonzo vilivyoteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure, na baadaye kuhakikiwa na Chandler na pia Wamitila. Mihimili ya nadharia hii ilitumika kuchambua mikakati iliyotumiwa na Gado katika vibonzo vyake kwa minajili ya kuendeleza maudhui ya kitashtiti. Utafiti huu ni wa kimaelezo na ulifanyika mtandaoni, pale ambapo mtafiti alipekua tovuti ya Gado (www.gadocartoons.com) na kuteua kimaksudi vibonzo vinane kutokana na jumla ya vibonzo ishirini vilivyokuwa vimechapishwa katika mwaka wa 2017. Uteuzi huu ulijikita katika vibonzo vilivyofungamana na madhumuni ya utafiti huu. Kwa jumla, utafiti huu ulidhibitisha kuwa mwanakibonzo Gado alitumia mbinu za lugha kama vile; kinaya, kejeli, metonimia, sitiara, analojia na mwingiliano matini kama mikakati ya kuibua kitashtiti katika vibonzo vyake. Vilevile, utafiti huu ulionyesha kuwa Gado alitumia ishara kama vile; matumizi ya rangi mbalimbali, pamoja na alama kama vile; heshtegi, mviringo na nyota kama mikakati ya kuibua tashtiti katika vibonzo vyake. Mwishowe, utafiti huu ulidhibitisha kuwa vibonzo vilivyochapishwa kwenye mtandao, vilidhihirisha uhuru na ukali mwingi katika usawiri wa masuala mbalimbali, jambo ambalo lilisaidia katika kufanikisha lengo kuu la tashtiti; ambalo ni ushambulizi unaochochea mabadiliko. Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yalitarajiwa kuwanufaisha wanamawasiliano, wanasemiotiki na wasomi wa masuala ya kisiasa kwa kuwapa mtazamo mpya kuhusiana na matumizi ya maneno na ishara katika kusimba jumbe tata zinazochapishwa kwenye mtandao ambapo kuna uhuru mwingi wa kuelezea masuala tata bila kudhibitiwa.","PeriodicalId":500309,"journal":{"name":"East African journal of Swahili studies","volume":"38 2","pages":""},"PeriodicalIF":0.0000,"publicationDate":"2024-01-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":"0","resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":null,"PeriodicalName":"East African journal of Swahili studies","FirstCategoryId":"0","ListUrlMain":"https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1685","RegionNum":0,"RegionCategory":null,"ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":null,"EPubDate":"","PubModel":"","JCR":"","JCRName":"","Score":null,"Total":0}
引用次数: 0
Abstract
Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizoweza kusemwa wazi wazi. Ifahamike kuwa sifa kuu ya vibonzo vya kisiasa ni kuwa vinapaswa kuwa cheshi na vyenye tashtiti ndiposa viweze kuwasilisha masuala tata kwa njia ya kimzaha. Kutokana na hali hii, utafiti huu ulichunguza tashtiti katika vibonzo vya kisiasa vya Gado vilivyochapishwa katika mwaka wa 2017 kwenye tovuti yake. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kupambanua mikakati iliyotumika katika kuendeleza maudhui ya kitashtiti katika vibonzo vilivyoteuliwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure, na baadaye kuhakikiwa na Chandler na pia Wamitila. Mihimili ya nadharia hii ilitumika kuchambua mikakati iliyotumiwa na Gado katika vibonzo vyake kwa minajili ya kuendeleza maudhui ya kitashtiti. Utafiti huu ni wa kimaelezo na ulifanyika mtandaoni, pale ambapo mtafiti alipekua tovuti ya Gado (www.gadocartoons.com) na kuteua kimaksudi vibonzo vinane kutokana na jumla ya vibonzo ishirini vilivyokuwa vimechapishwa katika mwaka wa 2017. Uteuzi huu ulijikita katika vibonzo vilivyofungamana na madhumuni ya utafiti huu. Kwa jumla, utafiti huu ulidhibitisha kuwa mwanakibonzo Gado alitumia mbinu za lugha kama vile; kinaya, kejeli, metonimia, sitiara, analojia na mwingiliano matini kama mikakati ya kuibua kitashtiti katika vibonzo vyake. Vilevile, utafiti huu ulionyesha kuwa Gado alitumia ishara kama vile; matumizi ya rangi mbalimbali, pamoja na alama kama vile; heshtegi, mviringo na nyota kama mikakati ya kuibua tashtiti katika vibonzo vyake. Mwishowe, utafiti huu ulidhibitisha kuwa vibonzo vilivyochapishwa kwenye mtandao, vilidhihirisha uhuru na ukali mwingi katika usawiri wa masuala mbalimbali, jambo ambalo lilisaidia katika kufanikisha lengo kuu la tashtiti; ambalo ni ushambulizi unaochochea mabadiliko. Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yalitarajiwa kuwanufaisha wanamawasiliano, wanasemiotiki na wasomi wa masuala ya kisiasa kwa kuwapa mtazamo mpya kuhusiana na matumizi ya maneno na ishara katika kusimba jumbe tata zinazochapishwa kwenye mtandao ambapo kuna uhuru mwingi wa kuelezea masuala tata bila kudhibitiwa.