Kimathi Mwembu, Allan Mugambi, Timothy Kinoti M’Ngaruthi
Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji, uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia.
{"title":"Ubadili Maana katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Kifonolojia na Kimofolojia","authors":"Kimathi Mwembu, Allan Mugambi, Timothy Kinoti M’Ngaruthi","doi":"10.37284/jammk.5.1.860","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.860","url":null,"abstract":"Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji, uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"16 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-09-26","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"115919937","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Makala hii inahakiki taswira ya mwanamke wa Kiswahili katika Utenzi wa Mwanakupona kwa kuzingatia utamaduni wa Waswahili wa karne ya kumi na tisa, ambao ndio wakati uliotungwa utenzi huu. Picha ya mwanamke huyu imehakikiwa kwa namna ambavyo inamulika mwanamke wa Kiswahili wa karne hiyo. Pamoja na kuusoma Utenzi wa Mwanakupona, tutahakiki kuhusu utenzi huu, na maandishi kuhusu utamaduni wa Waswahili wa karne ya kumi na tisa, mtafiti aliwahoji Waswahili watajika, wake kwa waume, kuhusu mwanamke katika utamaduni wa Waswahili. Pia, aliwasaili washairi wasifika na wanawake wa Kiswahili kuhusu uelewa wao wa utenzi huu. Yote haya kwa pamoja yalitoa mwanga kuhusu nafasi ya mwanamke katika utenzi huu maarufu. Nadharia ya uhalisia ilitumikizwa katika uhakiki huu na ilibainika kuwa mwanamke katika Utenzi wa Mwanakupona ni picha halisi ya mwanamke wa tabaka la juu, wa karne ya kumi na tisa.
{"title":"Mwanamke wa Kiswahili katika Utenzi wa Mwanakupona","authors":"S. Wandera-Simwa","doi":"10.37284/jammk.4.1.422","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.4.1.422","url":null,"abstract":"Makala hii inahakiki taswira ya mwanamke wa Kiswahili katika Utenzi wa Mwanakupona kwa kuzingatia utamaduni wa Waswahili wa karne ya kumi na tisa, ambao ndio wakati uliotungwa utenzi huu. Picha ya mwanamke huyu imehakikiwa kwa namna ambavyo inamulika mwanamke wa Kiswahili wa karne hiyo. Pamoja na kuusoma Utenzi wa Mwanakupona, tutahakiki kuhusu utenzi huu, na maandishi kuhusu utamaduni wa Waswahili wa karne ya kumi na tisa, mtafiti aliwahoji Waswahili watajika, wake kwa waume, kuhusu mwanamke katika utamaduni wa Waswahili. Pia, aliwasaili washairi wasifika na wanawake wa Kiswahili kuhusu uelewa wao wa utenzi huu. Yote haya kwa pamoja yalitoa mwanga kuhusu nafasi ya mwanamke katika utenzi huu maarufu. Nadharia ya uhalisia ilitumikizwa katika uhakiki huu na ilibainika kuwa mwanamke katika Utenzi wa Mwanakupona ni picha halisi ya mwanamke wa tabaka la juu, wa karne ya kumi na tisa.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"5 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-09-22","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"117043623","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Makala haya yalitalii uamilifu wa kipragmatiki wa kirai nomino katika sintaksia ya Kiswahili. Pragmatiki hujihusisha na namna watu wanavyotumia lugha katika muktadha na hali halisi ya mawasiliano. Hivyo basi, pragmatiki ni taaluma inayochunguza maana kulingana na muktadha fulani. Miongoni mwa maana za kimuktadha zilizoshughulikiwa ni pamoja na: maana dhanishi, maana tagusanishi na maana matinishi. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Sarufi Amilifu Mfumo (SAM) iliyopendekezwa na Halliday. Umuhimu wake ni kwamba inaeleza jinsi lugha inavyotumika katika hali halisi ya mawasiliano. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni mahojiano na uchunzaji. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu hizi zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikisawazisha mapungufu ya nyingine. Data ya maktabani ilitumika kuweka misingi ya ukusanyaji wa data ya nyanjani ambayo ilikusanywa kwa maswali ya mahojiano. Data katika makala haya ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya majedwali na maelezo. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Makala haya yaliweka bayana namna kirai nomino kinavyoweza kutumika kufumba ujumbe kipragmatiki katika mawasiliano. Makala haya yanatoa nafasi ya kupigiwa mfano ya kuchangia katika taaluma ya pragmatiki na isimu kwa jumla.
{"title":"Uamilifu wa Kipragmatiki wa Kirai Nomino (KN) Katika Kiswahili","authors":"Chege Joel Ngari","doi":"10.37284/jammk.5.1.853","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.853","url":null,"abstract":"Makala haya yalitalii uamilifu wa kipragmatiki wa kirai nomino katika sintaksia ya Kiswahili. Pragmatiki hujihusisha na namna watu wanavyotumia lugha katika muktadha na hali halisi ya mawasiliano. Hivyo basi, pragmatiki ni taaluma inayochunguza maana kulingana na muktadha fulani. Miongoni mwa maana za kimuktadha zilizoshughulikiwa ni pamoja na: maana dhanishi, maana tagusanishi na maana matinishi. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Sarufi Amilifu Mfumo (SAM) iliyopendekezwa na Halliday. Umuhimu wake ni kwamba inaeleza jinsi lugha inavyotumika katika hali halisi ya mawasiliano. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni mahojiano na uchunzaji. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu hizi zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikisawazisha mapungufu ya nyingine. Data ya maktabani ilitumika kuweka misingi ya ukusanyaji wa data ya nyanjani ambayo ilikusanywa kwa maswali ya mahojiano. Data katika makala haya ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya majedwali na maelezo. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Makala haya yaliweka bayana namna kirai nomino kinavyoweza kutumika kufumba ujumbe kipragmatiki katika mawasiliano. Makala haya yanatoa nafasi ya kupigiwa mfano ya kuchangia katika taaluma ya pragmatiki na isimu kwa jumla.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"56 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-09-21","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"131581633","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchunguzi huu kwa sababu ndio kamusi ya kwanza ya Sheng’ kuwahi kuchapishwa. Licha ya kamusi hii kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza ina leksimu za Sheng’ ambazo yafaa kuchunguzwa namna zinavyoathiri Kiswahili sanifu. Lengo la utafiti huu lilikuwa kubainisha maneno yaliyomo kwa Sheng’- English Dictionary na katika Kiswahili sanifu. Nadharia ya utafiti ilikuwa Nadharia ya Fonolojia Boreshi ambayo inapatikana katika mtazamo mpana wa Nadharia Boreshi iliyoasisiwa na Alan Prince na Paul Smolensky (1991). Hii ni nadharia inayochunguza hatua za ukuaji wa msamiati kutoka hali ghafi hadi ukubalifu wake kupitia kwa vizuizi tofauti. Mahali pa utafiti palikuwa maktabani na mtandaoni. Mbinu ya uchunguzi ikawa kupitia kusikiliza na kusoma makala mbalimbali kuhusu mada hii. Data ilikusanywa kupitia kwa kuchunguza maneno na vidahizo vya maneno kutoka kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003). Iliaminika kuwa kamusi hii ingetupa sampuli ya maneno mahsusi ya Sheng’ ambayo muundo wake huathiri matumizi katika Kiswahili sanifu kwenye jamii ya kisasa. Uchanganuzi wa maelezo ulitegemea mtazamo wa Fonolojia Boreshi katika nadharia ya fonolojia inayoangazia sarufi zalishi. Katika mtazamo huu, uambishaji wa maneno uliangaziwa na jinsi uundaji huo hutawaliwa na vizuizi mbalimbali na sheria za fonolojia. Uwasilishaji wa data ulikuwa kupitia kwa maelezo ya kina, michoro na jedwali. Uchunguzi huu ulidhamiria kuchangia usomi wa Kiswahili kwa kuweka wazi athari za Sheng’ katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimsamiati. Kadhalika, utafiti huu utawasaidia wanafunzi kuweka mipaka bayana kati ya msimbo wa Sheng’ na lugha ya Kiswahili sanifu.
{"title":"Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu","authors":"Jotham Muyumba, David Kihara","doi":"10.37284/jammk.5.1.827","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.827","url":null,"abstract":"Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchunguzi huu kwa sababu ndio kamusi ya kwanza ya Sheng’ kuwahi kuchapishwa. Licha ya kamusi hii kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza ina leksimu za Sheng’ ambazo yafaa kuchunguzwa namna zinavyoathiri Kiswahili sanifu. Lengo la utafiti huu lilikuwa kubainisha maneno yaliyomo kwa Sheng’- English Dictionary na katika Kiswahili sanifu. Nadharia ya utafiti ilikuwa Nadharia ya Fonolojia Boreshi ambayo inapatikana katika mtazamo mpana wa Nadharia Boreshi iliyoasisiwa na Alan Prince na Paul Smolensky (1991). Hii ni nadharia inayochunguza hatua za ukuaji wa msamiati kutoka hali ghafi hadi ukubalifu wake kupitia kwa vizuizi tofauti. Mahali pa utafiti palikuwa maktabani na mtandaoni. Mbinu ya uchunguzi ikawa kupitia kusikiliza na kusoma makala mbalimbali kuhusu mada hii. Data ilikusanywa kupitia kwa kuchunguza maneno na vidahizo vya maneno kutoka kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003). Iliaminika kuwa kamusi hii ingetupa sampuli ya maneno mahsusi ya Sheng’ ambayo muundo wake huathiri matumizi katika Kiswahili sanifu kwenye jamii ya kisasa. Uchanganuzi wa maelezo ulitegemea mtazamo wa Fonolojia Boreshi katika nadharia ya fonolojia inayoangazia sarufi zalishi. Katika mtazamo huu, uambishaji wa maneno uliangaziwa na jinsi uundaji huo hutawaliwa na vizuizi mbalimbali na sheria za fonolojia. Uwasilishaji wa data ulikuwa kupitia kwa maelezo ya kina, michoro na jedwali. Uchunguzi huu ulidhamiria kuchangia usomi wa Kiswahili kwa kuweka wazi athari za Sheng’ katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimsamiati. Kadhalika, utafiti huu utawasaidia wanafunzi kuweka mipaka bayana kati ya msimbo wa Sheng’ na lugha ya Kiswahili sanifu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"90 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-09-06","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"121485532","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Lugha zote ulimwenguni huwa na sheria zake zinazohusu mfuatano wa maneno katika sentensi. Hivyo basi, kama zilivyo lugha zingine, lugha ya Kiswahili vilevile ina utaratibu mwafaka ambao vivumishi katika kirai nomino (KN) hufuata ili kuibua sentensi kubalifu sio kimantiki tu, bali pia kisarufi, jambo ambalo huathiri maana ya KN husika. Makala haya yameweka bayana utaratibu wa vipengele vya kirai nomino katika Kiswahili. Nadharia ya Eksibaa iliyoasisiwa na Noam Chomsky ilitumika. Nadharia ya Eksibaa ni nadharia ya muundo virai inayoonyesha kategoria za sintaksia zinazofungamanishwa na nomino. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni hojaji na mahojiano. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu husika zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikifidia mapungufu ya nyingine. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio. Utafiti huu ulishirikisha watafitiwa 120 ili kuafiki lengo husika. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makundi matatu ya utaratibu wa vipengele vya kirai nomino ambayo ni: kirai nomino cha kiwakilishi na vivumishi, kirai nomino chenye nomino vivumishi na kishazi tegemezi na mwisho ni kirai nomino cha nomino, kitenzi jina na kivumishi. Matokeo ya utafiti huu yatapanua uelewa wa kirai nomino kwa mitazamo tofauti na hivyo kuongeza maarifa kuhusiana na dhana husika. Vilevile, mapendekezo ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa wanafunzi, waandishi wa vitabu, Wizara ya Elimu, serikali, wapangaji mitaala, watafiti wa baadaye na walimu chipukizi kupanua ufahamu na uelewa wa tawi la isimu ambalo ni pragmatiki.
{"title":"Utaratibu wa Vipengele vya Kirai Nomino katika Kiswahili","authors":"Chege Joel Ngari, Leonard Chacha Mwita","doi":"10.37284/jammk.5.1.826","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.826","url":null,"abstract":"Lugha zote ulimwenguni huwa na sheria zake zinazohusu mfuatano wa maneno katika sentensi. Hivyo basi, kama zilivyo lugha zingine, lugha ya Kiswahili vilevile ina utaratibu mwafaka ambao vivumishi katika kirai nomino (KN) hufuata ili kuibua sentensi kubalifu sio kimantiki tu, bali pia kisarufi, jambo ambalo huathiri maana ya KN husika. Makala haya yameweka bayana utaratibu wa vipengele vya kirai nomino katika Kiswahili. Nadharia ya Eksibaa iliyoasisiwa na Noam Chomsky ilitumika. Nadharia ya Eksibaa ni nadharia ya muundo virai inayoonyesha kategoria za sintaksia zinazofungamanishwa na nomino. Mbinu za utafiti zilizoongoza utafiti huu ni hojaji na mahojiano. Mbinu ya uchunzaji ilitumika ambapo maongezi ya wazungumzaji yalirekodiwa. Mbinu husika zilikamilishana na kujengana kila mojawazo ikifidia mapungufu ya nyingine. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio. Utafiti huu ulishirikisha watafitiwa 120 ili kuafiki lengo husika. Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni: wahadhiri na walimu, vijana waliomaliza shule ya upili na vyuo na wanafunzi wa shule za upili na vyuo. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha makundi matatu ya utaratibu wa vipengele vya kirai nomino ambayo ni: kirai nomino cha kiwakilishi na vivumishi, kirai nomino chenye nomino vivumishi na kishazi tegemezi na mwisho ni kirai nomino cha nomino, kitenzi jina na kivumishi. Matokeo ya utafiti huu yatapanua uelewa wa kirai nomino kwa mitazamo tofauti na hivyo kuongeza maarifa kuhusiana na dhana husika. Vilevile, mapendekezo ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa wanafunzi, waandishi wa vitabu, Wizara ya Elimu, serikali, wapangaji mitaala, watafiti wa baadaye na walimu chipukizi kupanua ufahamu na uelewa wa tawi la isimu ambalo ni pragmatiki.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"18 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-09-05","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"123074205","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Nyimbo zikiwa za watoto, inatarajiwa kuwa walengwa watakuwa watoto wenyewe kwa kuwa maudhui yaliyomo yatawalenga. Bembelezi zilizotafitiwa katika tamaduni mbalimbali ulimwenguni zinaonyesha kuwa ujumbe uliyomo huwalenga watoto na wakati mwingine, mama na baba zao. Kimsingi, wanawake, kando na kuzitumia katika shughuli za kubembeleza watoto, huzitumia pia kama jukwaa la kujieleza na kutakasa mioyo yao kutokana na uchungu, mtamauko na mfadhaiko wa mawazo uliosababishwa na matatizo ya kindoa kutokana na mifumo ya kibabedume inayoendelezwa katika baadhi ya jamii. Makala hii inachunguza diskosi zinazojitokeza katika bembelezi za Watikuu ili kubaini walengwa wa ujumbe uliomo. Lugha inayotumiwa na wanawake katika uimbaji wa bembelezi hizi inatilia shaka iwapo ujumbe uliomo unalenga tu watoto au mna watu wengine wanaolengwa kando na watoto.
Nyimbo zikiwa za watoto, inatarajiwa kuwa walengwa watakuwa watoto wenyewe kuwa maudhui yaliyomo yatawalenga.本贝莱兹(Bembelezi)的 "zilizotafitiwa katika tamaduni mbalimbali ulimwenguni zinaonyesha kuwa ujumbe uliyomo huwalenga watoto na wakati mwingine, mama na baba zao"。在这些人中,有的人被认为是 "糊涂虫",有的人被认为是 "糊涂虫",有的人被认为是 "糊涂虫",有的人被认为是 "糊涂虫",有的人被认为是 "糊涂虫",有的人被认为是 "糊涂虫"。我们的目标是:通过我们的努力,使我们的国家成为世界上最强大的国家之一。这就要求我们在教育孩子时,要以孩子为本,以孩子的发展为本,以孩子的健康为本,以孩子的快乐为本,以孩子的幸福为本,以孩子的健康为本。
{"title":"Walengwa wa Ujumbe katika Bembelezi za Watikuu","authors":"Lina Akaka, Sheila Wandera- Simwa","doi":"10.37284/jammk.5.1.817","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.817","url":null,"abstract":"Nyimbo zikiwa za watoto, inatarajiwa kuwa walengwa watakuwa watoto wenyewe kwa kuwa maudhui yaliyomo yatawalenga. Bembelezi zilizotafitiwa katika tamaduni mbalimbali ulimwenguni zinaonyesha kuwa ujumbe uliyomo huwalenga watoto na wakati mwingine, mama na baba zao. Kimsingi, wanawake, kando na kuzitumia katika shughuli za kubembeleza watoto, huzitumia pia kama jukwaa la kujieleza na kutakasa mioyo yao kutokana na uchungu, mtamauko na mfadhaiko wa mawazo uliosababishwa na matatizo ya kindoa kutokana na mifumo ya kibabedume inayoendelezwa katika baadhi ya jamii. Makala hii inachunguza diskosi zinazojitokeza katika bembelezi za Watikuu ili kubaini walengwa wa ujumbe uliomo. Lugha inayotumiwa na wanawake katika uimbaji wa bembelezi hizi inatilia shaka iwapo ujumbe uliomo unalenga tu watoto au mna watu wengine wanaolengwa kando na watoto.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"11 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-08-26","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"131855450","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Eliud Miriti Josphat, N. Gitonga, Dorcas M. Musyimi
Waigembe wana utamaduni ambao unafungamana na nyimbo ambazo zinaimbwa katika hafla tofauti tofauti. Nyimbo za tohara pamoja na nyimbo za kidini za Kikristo ni baadhi ya zile zinaimbwa. Nyimbo za tohara zinaimbwa wakati wa kutahiri wavulana na za kidini wakati wa shughuli za kidini ya Kikristo. Hata hivyo, hatua ya waimbaji wa nyimbo za dini ya Kikristo kubadilisha nyimbo za tohara kimaudhui, kimtindo na kiutendakazi ili kuzitumia upya katika mazingira ya kidini ili kusaidia katika maenezi ya injili ya Kikristo kwa wengi na kutumika katika hafla zingine za kijamii kando na tohara ni jambo ambalo ni mpya katika jamii ya Waigembe. Hiki ndicho kiliwachochea watafiti kutafiti udenguzi wa nyimbo za tohara za Waigembe na nyimbo za dini ya Kikristo ili kuweza kutumika katika hafla tofauti kando na tohara. Makala haya yalilenga kubainisha maudhui ambayo nyimbo za tohara zilizodenguliwa na nyimbo za dini ya Kikristo huwa nayo katika jamii ya Waigembe. Watafiti waliongozwa na nadharia ya udenguzi. Data ya nyimbo kumi na nane imetumika katika makala haya. Awamu tatu ambazo nyimbo hizo hufuata zilichanganuliwa na kuwasilisha maudhui kwa njia ya maelezo. Makala haya yanachangia katika kuongeza maarifa ya kiutafiti kuhusu nyimbo zilizodenguliwa za tohara za Kiigembe, pamoja na kuhifadhi fasihi simulizi ya Kiafrika ili itumike na vizazi vijavyo katika kuafikia maendeleo endelevu.
{"title":"Maudhui Katika Nyimbo za Tohara Zilizodenguliwa na Nyimbo za Dini za Kiigembe katika Kuafikia Maendeleo Endelevu kwa Waigembe","authors":"Eliud Miriti Josphat, N. Gitonga, Dorcas M. Musyimi","doi":"10.37284/jammk.5.1.813","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.813","url":null,"abstract":"Waigembe wana utamaduni ambao unafungamana na nyimbo ambazo zinaimbwa katika hafla tofauti tofauti. Nyimbo za tohara pamoja na nyimbo za kidini za Kikristo ni baadhi ya zile zinaimbwa. Nyimbo za tohara zinaimbwa wakati wa kutahiri wavulana na za kidini wakati wa shughuli za kidini ya Kikristo. Hata hivyo, hatua ya waimbaji wa nyimbo za dini ya Kikristo kubadilisha nyimbo za tohara kimaudhui, kimtindo na kiutendakazi ili kuzitumia upya katika mazingira ya kidini ili kusaidia katika maenezi ya injili ya Kikristo kwa wengi na kutumika katika hafla zingine za kijamii kando na tohara ni jambo ambalo ni mpya katika jamii ya Waigembe. Hiki ndicho kiliwachochea watafiti kutafiti udenguzi wa nyimbo za tohara za Waigembe na nyimbo za dini ya Kikristo ili kuweza kutumika katika hafla tofauti kando na tohara. Makala haya yalilenga kubainisha maudhui ambayo nyimbo za tohara zilizodenguliwa na nyimbo za dini ya Kikristo huwa nayo katika jamii ya Waigembe. Watafiti waliongozwa na nadharia ya udenguzi. Data ya nyimbo kumi na nane imetumika katika makala haya. Awamu tatu ambazo nyimbo hizo hufuata zilichanganuliwa na kuwasilisha maudhui kwa njia ya maelezo. Makala haya yanachangia katika kuongeza maarifa ya kiutafiti kuhusu nyimbo zilizodenguliwa za tohara za Kiigembe, pamoja na kuhifadhi fasihi simulizi ya Kiafrika ili itumike na vizazi vijavyo katika kuafikia maendeleo endelevu.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"26 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-08-25","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"115760771","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Lahaja za kiAmu, kiMvit̪a zafa, na lahaja nyenginezo za kiSwahili yasemekana zishakufa. Makala haya yanaonesha kuwa usuli wa matatizo haya ni mapungufu ya juhud̪i za kukisanifisha kiSwahili wakat̪i wa ukoloni. Vigezo va uwamilifu wa kut̪afaut̪isha maana, na kiwango cha matumizi wa saut̪i hiyo katika lugha, ni mambo yaliyopuuzwa na Kamati ya Lugha kwa sababu ya kut̪afut̪a unafuu wa kusanifisha. Tukifuwatʰa nadhariya-tʰetʰe ya Kina cha Othografiya, saut̪i hizi amilifu tumeziyonesha kuwa zachʰangiya katika kusoma maand̪ishi yaliyoand̪ikwa kwa sababu kiSwahili ni lugha yenye othografiya ya maonroni, yaani, kuna mnasaba wa moja kwa moja kati ya saut̪i na kiwakilishi chake kihati; kitamkwavo nrivo kiyand̪ikwavo. Kwengezeya, mfumuko wa TEKNOHAMA umeipa t̪ena, lugha ya kiSwahili, nafasi ya kufaid̪ika na saut̪i hizi kwa kutiya kila kʰitʰu katika nukt̪̪a ya kimahesabu hivo kurahisisha utambuzi wa saut̪i hizi na urahisi wa kuzitumiya katika masomi ya shuleni na kwenye t̪afsiri mashine ya makala ya kiSwahili. Ikawa nat̪ija ipatikanayo ni kukiokowa kiSanifu kut̪okana na kuziokowa lahaja dada zake. Lakini zaid̪i, ni kupatikana ut̪angamano wa lugha zot̪ʰe nchini Kenya na utambulisho muwafaka katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
我们的工作是:为非洲人、为非洲人的生活、为非洲人的语言、为非洲人的社会、为非洲人的文化、为非洲人的社会、为非洲人的生活、为非洲人的社会、为非洲人的社会、为非洲人的社会、为非洲人的社会、为非洲人的社会、为非洲人的社会、为非洲人的社会、为非洲人的社会、为非洲人的社会、为非洲人的社会。我们还将继续努力,使我们的语言在世界范围内发挥更大的作用。如果您想了解更多关于 "库克萨尼法 "的信息,请联系我们,我们将竭诚为您服务。在""(Tukifuwatʰa nadhariya-tʰetʰe ya Kina cha Othografiya, saut̪i hizi amilifu tumeziyonesha kuwa zachʰangiya katika kusoma maand̪ishi yaliyoand̪ikwa kwa sababu kiSwahili ni lugha yenye othografiya ya maonroni, yaani, kuna mnasaba wa moja kwa moja kati ya saut̪i na kiwakilishi chake kihati;kitamkwavo nrivo kiyand̪ikwavo。Kwengezeya, mfumuko wa TEKNOHAMA umeipa t̪ena, lugha ya kiSwahili、我们的目标是:在我们的国家,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区,在我们的社区。在斯瓦希里语中,"ipatikanayo"(ipatikanayo)与 "kukiokowa kiSanifu kut̪okana"(ipatikanayo)同音,"kuziokowa lahaja dada zake"(ipatikanayo)同义。在肯尼亚,有一个名为 "马沙里基非洲之友 "的组织。
{"title":"Ufungamanisho wa Fonolojiya Othografiya na Teknolojiya katika Kukiyand̪ika Upya Kiswahili Sanifu; Kujiokowa na Kuokowa Mustakabali wa Lahaja-Dadaze","authors":"M. Karama","doi":"10.37284/jammk.5.1.803","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.803","url":null,"abstract":"Lahaja za kiAmu, kiMvit̪a zafa, na lahaja nyenginezo za kiSwahili yasemekana zishakufa. Makala haya yanaonesha kuwa usuli wa matatizo haya ni mapungufu ya juhud̪i za kukisanifisha kiSwahili wakat̪i wa ukoloni. Vigezo va uwamilifu wa kut̪afaut̪isha maana, na kiwango cha matumizi wa saut̪i hiyo katika lugha, ni mambo yaliyopuuzwa na Kamati ya Lugha kwa sababu ya kut̪afut̪a unafuu wa kusanifisha. Tukifuwatʰa nadhariya-tʰetʰe ya Kina cha Othografiya, saut̪i hizi amilifu tumeziyonesha kuwa zachʰangiya katika kusoma maand̪ishi yaliyoand̪ikwa kwa sababu kiSwahili ni lugha yenye othografiya ya maonroni, yaani, kuna mnasaba wa moja kwa moja kati ya saut̪i na kiwakilishi chake kihati; kitamkwavo nrivo kiyand̪ikwavo. Kwengezeya, mfumuko wa TEKNOHAMA umeipa t̪ena, lugha ya kiSwahili, nafasi ya kufaid̪ika na saut̪i hizi kwa kutiya kila kʰitʰu katika nukt̪̪a ya kimahesabu hivo kurahisisha utambuzi wa saut̪i hizi na urahisi wa kuzitumiya katika masomi ya shuleni na kwenye t̪afsiri mashine ya makala ya kiSwahili. Ikawa nat̪ija ipatikanayo ni kukiokowa kiSanifu kut̪okana na kuziokowa lahaja dada zake. Lakini zaid̪i, ni kupatikana ut̪angamano wa lugha zot̪ʰe nchini Kenya na utambulisho muwafaka katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"1 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-08-24","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"130286478","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Asca Monica Koko, Juliet Akinyi Jagero, N. N. Musembi
Matamko tendi (MT) ni vitendo vinavyotekelezwa kwa kuvitamka tu kwa sauti. Katika matamko tendi msemaji huwa ametenda kupitia kuzungumza. Riwaya inatarajiwa kuwa na usimulizi hata hivyo dayolojia huweza kutokea katika riwaya. Kutokana na hayo, makala hii inanuia kuchunguza matamko tendi yanayopatikana katika dayolojia baina ya wahusika katika riwaya za Walibora. Makala hii inalenga kuchanganua matamko tendi na athari zake katika riwaya za Walibora. Makala iliongozwa na Nadharia ya Vitendo usemi. Sampuli dhamirifu ilitumika kuteua riwaya nne za Walibora huku sampuli dabwadabwa ikitumika kuteua MT kutoka riwaya hizo. Mbinu ya unukuzi ilitumiwa kudondoa sehemu za matini na kuwekwa kwenye jedwali la matukio. Data zilichanganuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo kulingana na madhumuni ya makala na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Makala ilionyesha kwamba wahusika waliathiriwa na matamko kwa njia chanya hasa matamko ya furaha na kujenga mahusiano katika jamii. Uchanganuzi wa MT una umuhimu katika usomaji, uchanganuzi na ufasiriaji wa mazungumzo ya wahusika na maana anayonuia mwandishi wa Riwaya.
{"title":"Matamko Tendi na Athari Zake kwa Wahusika katika Riwaya za Ken Walibora","authors":"Asca Monica Koko, Juliet Akinyi Jagero, N. N. Musembi","doi":"10.37284/jammk.5.1.799","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.799","url":null,"abstract":"Matamko tendi (MT) ni vitendo vinavyotekelezwa kwa kuvitamka tu kwa sauti. Katika matamko tendi msemaji huwa ametenda kupitia kuzungumza. Riwaya inatarajiwa kuwa na usimulizi hata hivyo dayolojia huweza kutokea katika riwaya. Kutokana na hayo, makala hii inanuia kuchunguza matamko tendi yanayopatikana katika dayolojia baina ya wahusika katika riwaya za Walibora. Makala hii inalenga kuchanganua matamko tendi na athari zake katika riwaya za Walibora. Makala iliongozwa na Nadharia ya Vitendo usemi. Sampuli dhamirifu ilitumika kuteua riwaya nne za Walibora huku sampuli dabwadabwa ikitumika kuteua MT kutoka riwaya hizo. Mbinu ya unukuzi ilitumiwa kudondoa sehemu za matini na kuwekwa kwenye jedwali la matukio. Data zilichanganuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo kulingana na madhumuni ya makala na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na majedwali. Makala ilionyesha kwamba wahusika waliathiriwa na matamko kwa njia chanya hasa matamko ya furaha na kujenga mahusiano katika jamii. Uchanganuzi wa MT una umuhimu katika usomaji, uchanganuzi na ufasiriaji wa mazungumzo ya wahusika na maana anayonuia mwandishi wa Riwaya.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"29 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-08-19","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"122144325","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}
Beatrice Nyambura Njeru, John M. Kobia, Allan Mugambi
Wahusika ni viumbe muhimu katika ujenzi wa kazi ya fasihi. Mhusika ni mtendaji katika kazi ya kifasihi na huwa ni kielelezo cha viumbe wanaopatikana ulimwenguni ingawa si lazima sifa zote za mhusika zifungamane na za binadamu. Ni picha ambayo huchorwa na fasihi na ni kiini cha vitu vipya, dhamira na mada katika fasihi. Kwa hivyo, wahusika si watu halisi bali ni watu wa kubuni. Mwandishi huchora viumbe anaowatwika majukumu ya kutenda na kusema kama binadamu na kupitia kwao huwasilisha dhamira yake. Dhamira hii hukuzwa na kuwepo kwa masuala makuu ambayo huwasilishwa kwa hadhira lengwa na kufanikisha lengo kuu la utunzi wa kazi ya fasihi. Makala haya yanalenga kuchunguza namna ambavyo wahusika huingiliana kutoka kwa matini moja hadi nyingine katika nathari teule za fasihi ya Kiswahili. Mwingilianomatini hubainisha kuwa matini moja inaweza kuhusiana na matini nyingine katika viwango mbalimbali kama vile usawiri wa wahusika, usawiri wa mandhari, maudhui na mtindo wa uandishi. Sampuli maksudi ilitumika kuteua vitabu saba kwa msingi kuwa vina dhana ya siri katika uteuzi wa mada. Vitabu hivi ambavyo ni Nataka Iwe Siri, Sitaki Iwe Siri, Siri Ya Baba Yangu Kitabu 1, Siri Ya Baba Yangu 2, Siri Sirini 1, Siri Sirini 2 na Siri Sirini 3 vimedhihirisha kuwa kuna siri ambazo zimejengwa na wahusika katika bunilizi teule na kufanikisha motifu ya siri. Uchanganuzi na uwasilishwaji wa data itakayopatikana kutokana na usomaji wa kazi teule utakuwa wa kimaelezo. Makala haya yatawafaa wahakiki kwa kuwapa mwanga wa namna ya kuhakiki kazi zinazohusiana na siri na kuchunguza namna wahusika wanavyoweza kuingiliana kwa namna tofauti na kufanikisha ujenzi wa motifu ya siri. Aidha walimu na wanafunzi wa viwango vyote watafaidika kwa sababu wataelewa kazi teule zaidi. Waandishi nao watafaidika kutokana na makala haya kwa sababu watayatumia kama kifaa cha kutunga kazi za baadaye za kiwango cha juu zaidi kuhusiana na motifu ya siri. Vilevile makala haya yatatoa mchango mkubwa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili kwa kuwa yataongeza maarifa mapya kuhusu namna wahusika wanaweza kuingiliana na kukuza kazi za kibunilizi zilizo na motifu mbalimbali.
{"title":"Wahusika na Motifu ya Siri katika Nathari Teule za Fasihi za Kiswahili","authors":"Beatrice Nyambura Njeru, John M. Kobia, Allan Mugambi","doi":"10.37284/jammk.5.1.782","DOIUrl":"https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.782","url":null,"abstract":"Wahusika ni viumbe muhimu katika ujenzi wa kazi ya fasihi. Mhusika ni mtendaji katika kazi ya kifasihi na huwa ni kielelezo cha viumbe wanaopatikana ulimwenguni ingawa si lazima sifa zote za mhusika zifungamane na za binadamu. Ni picha ambayo huchorwa na fasihi na ni kiini cha vitu vipya, dhamira na mada katika fasihi. Kwa hivyo, wahusika si watu halisi bali ni watu wa kubuni. Mwandishi huchora viumbe anaowatwika majukumu ya kutenda na kusema kama binadamu na kupitia kwao huwasilisha dhamira yake. Dhamira hii hukuzwa na kuwepo kwa masuala makuu ambayo huwasilishwa kwa hadhira lengwa na kufanikisha lengo kuu la utunzi wa kazi ya fasihi. Makala haya yanalenga kuchunguza namna ambavyo wahusika huingiliana kutoka kwa matini moja hadi nyingine katika nathari teule za fasihi ya Kiswahili. Mwingilianomatini hubainisha kuwa matini moja inaweza kuhusiana na matini nyingine katika viwango mbalimbali kama vile usawiri wa wahusika, usawiri wa mandhari, maudhui na mtindo wa uandishi. Sampuli maksudi ilitumika kuteua vitabu saba kwa msingi kuwa vina dhana ya siri katika uteuzi wa mada. Vitabu hivi ambavyo ni Nataka Iwe Siri, Sitaki Iwe Siri, Siri Ya Baba Yangu Kitabu 1, Siri Ya Baba Yangu 2, Siri Sirini 1, Siri Sirini 2 na Siri Sirini 3 vimedhihirisha kuwa kuna siri ambazo zimejengwa na wahusika katika bunilizi teule na kufanikisha motifu ya siri. Uchanganuzi na uwasilishwaji wa data itakayopatikana kutokana na usomaji wa kazi teule utakuwa wa kimaelezo. Makala haya yatawafaa wahakiki kwa kuwapa mwanga wa namna ya kuhakiki kazi zinazohusiana na siri na kuchunguza namna wahusika wanavyoweza kuingiliana kwa namna tofauti na kufanikisha ujenzi wa motifu ya siri. Aidha walimu na wanafunzi wa viwango vyote watafaidika kwa sababu wataelewa kazi teule zaidi. Waandishi nao watafaidika kutokana na makala haya kwa sababu watayatumia kama kifaa cha kutunga kazi za baadaye za kiwango cha juu zaidi kuhusiana na motifu ya siri. Vilevile makala haya yatatoa mchango mkubwa katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili kwa kuwa yataongeza maarifa mapya kuhusu namna wahusika wanaweza kuingiliana na kukuza kazi za kibunilizi zilizo na motifu mbalimbali.","PeriodicalId":112928,"journal":{"name":"East African Journal of Swahili Studies","volume":"2 1","pages":"0"},"PeriodicalIF":0.0,"publicationDate":"2022-08-08","publicationTypes":"Journal Article","fieldsOfStudy":null,"isOpenAccess":false,"openAccessPdf":"","citationCount":null,"resultStr":null,"platform":"Semanticscholar","paperid":"116956380","PeriodicalName":null,"FirstCategoryId":null,"ListUrlMain":null,"RegionNum":0,"RegionCategory":"","ArticlePicture":[],"TitleCN":null,"AbstractTextCN":null,"PMCID":"","EPubDate":null,"PubModel":null,"JCR":null,"JCRName":null,"Score":null,"Total":0}